Na. Cosmas Mathias Njingo.
GAIRO, Morogoro.
Novemba 2.2022
Wakati baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF, wakiendelea kuishi katika hali duni ya kimaisha kwa kushindwa kubuni na kuibua miradi ya kuchumi, hata baada ya Serikali kuwapatia ruzuku hiyo ili wawezesha kuondokana na umaskini kwa madai ya kupewa ruzuku kidogo. Mtazamo huo umepokelewa tofauti na Bi. Monica Philipo Mwite ambaye ameweza kutumia kiasi kidogo cha ruzuku hiyo kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi.
Bi. Monica Philipo Mwite akiwa pandani mwa kuku ambao aliwanunua kwa kuweka akiba kidogo kidogo za ruzuku ya kunusuru kaya Maskini TASAF (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO).
Bi. Mwite mama wa watoto 5, anayeishi na mama yake Mzazi mwenye ulemavu, amesema; pamoja na serikali kupitia TASAF inatoa ruzuku kidogo, lakini kwake ametumia ruzuku hiyo kuwekeza kwenye miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo imemuwezesha kuondokana na hali ya ufukara aliyokuwa nayo hapo awali.
“Ni kweli ruzuku haitoshi, lakini ninachokiona mimi, ni muhimu sana kwa wanufaika wenzangu wa mpango huu wa TASAF kuigawa ruzuku hiyo, badala ya kuitumia yote kwa mahitaji ya chakula. Mimi nilijiongeza, nikaona ni afadhali kutumia pesa kidogo na nyingine kutunza akiba ili nipate mtaji wa kuanzisha biashara.
Anasema hapo awali maisha yake yalikuwa magumu sana, lakini kupitia mpango huu, ameweza kufuga kuku wa nyama, kuuza vitunguu maji, mbogambona na viazi mviringo, biashara ambazo zimemsaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha yake na kupiga hatua kiuchumi.
Bi. Nonica Philipo Mwite, akihudumia vifaranga wa wakuku nyumbani kwake Mamuli, Kata ya Gairo (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Mbali na ufugaji wa kuku Bi. Mwite pia anajishughulisha na biashara ndogo ndogo za uuzaji wa mboga mboga, vitunguu, nyanya chungu na viazi mziringo biashara ambayo anasema huwa anazunguka kwenye magulio ya kila wiki katika maeneo mbalimbali Wilayani Gairo, lengo ikiwa anahakikisha anasogeza karibu huduma kwa wateja wake.
Bi. Monica akipamga bidhaa katika gulio la Ukwamani, Kata ya Ukwamani ambalo hufanyika kila siku za Alhamisi (Pcha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO).
Kwa upande mwingine anasema kuwa biashara ya kuuza mbogamboga pamoja na ufugaji wa kuku vimemuwezesha kuboresha miundombinu ya nyumba yake kwa kuongezea urefu kwenda juu na kupaua upya, kuvuta bomba la maji sambamba na kuvuta umeme.
“TASAF ni mombozi mkuwa sana kwa watu maskini kama mimi, ruzuku niliyoipata imenisaidia kuanzisha biashara ndogondogo, nimevuta maji na umeme, lakini pia nimeiongezea nyumba yangu kwenda juu maana ilikuwa kama kibanda cha kupumzika au chumba chamba za nje cha kupikia chakula”. Alisema.
Miundombinu ya Umeme katika nyumba iliyoboreshwa ya Bi. Monica (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Bi. Monica alianza kwa ruzuku ya Shilingi. 36,000 (elfu thelathini na sita), lakini kwa sasa ruzuku hiyo imeongezeka hadi kufikia shilingi 42,000 (arobaini na mbili elfu) na kwamba inamsaidia kujikimu kimaisha na kuendelea miradi yake.
Adha mnufaika huyo wa mpango wa kunusuru Kaya zaidi-TASAF amesema maeneleo ya watoto wake kitaaluma ni mazuri kwa kuwa anauwezo wa kuwahudumia na kutimiza mahitaji yao ikiwepo chakula cha mchana shuleni, viatu, nguo na madaftari.
Bi Monica akiwa na baadhi ya watoto na Wajukuu zake(Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Matarajio yake yabaadae ni kuwa mfugaji mkubwa wa kuku wa kienyeji ambao anasma atafuga kisasa zaidi ili kuhakikisha anazalisha kuku wa kutosha na kuongeza soko la ndani nan je ya Wilaya ya Gairo. Hadi sasa ana kuku wakubwa wanafikia 69, vifaranga 64 jumla ya kuku wote wanafikia 133 (miamoja thelathini na tatu), kati ya hao 5 wanataga mayai, wawili wanalea vifaranga.
Sehemu ya paa la nyumba baada ya kufantiwa maboresho ya kuongezewa urefu wa ukuta kwenda juu (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO).
Nishati ya umeme ikitumika, baada ya kufanya maboresho ya nyumba na kuvuta huduma ya umeme (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa