Na. Cosmas M. Njingo. Gairo Morogoro
Sept.2 2022
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro, imepokea jumla ya Vitabu 19080 vya masomo mbalimnali kwa ajili ya Kidato cha kwanza, pili na Tatu kutoka Taasisi ya Elimu (TEA) kwa ajili ya kusaidia shule za sekondari za Serikali.
Vitabu hivyo ni kwa ajili ya masomo ya Sayansi (Fizikia & Baiolojia), Hesabu, Tehama, Kiswahili, Jiografiana, na Uraia
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mwalimu Nevoneia Levery amasema msaada huo wa Vitabu ni mkombozi kwa Shule za Sekondari Wilayani humo na kwamba vitabu hivyo vitaongeza ari ya ujifunzi na ufundishaji na kuongeza kiwango cha ufaulu.
“Tumepokea Vitabu 19,080 vya masomo ya Sayansi, TEHAMA, Hisabati, Bioloji, Fizikia na Kemia kwa ajli ya Kidato cha Kwanza hadi kitado cha Nne kwa shule zetu za Sekondari. Vitabu hivi vinekuja wakwati muafaka sana. Tunatarajia vitaleta mapinduzi makubwa katika kuinua kiwango cha ufaulu kwa watoto wetu”.
Akikabidhi vitabu hivyo kwa Wakuu wa Shule na wawakilishi wa Wakuu wa Shule ambao hawakufika katika makabidhiano hayo, Mwalimu Levery aliwaambia Wakuu na wawakilishi hao kuhakikisha vitabu hivyo vinatumika vizuri ili malengo ya kuinua taaluma Wilayani humo yatime.
“Wito wangu kwa Wakuu wa Shule wote, wakahakikishe vitabu vinatumika vizuri na vinatunzwa kwa uangalifu ili kuhakikisha malengo yetu yanafikiwa. Tunahitaji kuona mapinduzi makubwa ya kitaaluma kwani tunamini vitabu hivi vitawawezesha watoto wetu kujisomea na kujifunza katika hali ya utulivu zaidi tofauti na awali ambapo vitabu vilikuwa havijitoshelezi”. Alisisitiza Afisa Elimu Levery.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Sekwao Mwalimu Anifa Kisimbo na Kaimu Mkuu wa Shule ye Sekondari Rubeho, Mwalimu Getrude Sawe, wakizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Shule waliishuruku Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa kutoa msaada huo wa Vitabu kwa ajili ya kuwezesha Wanafunzi wa Shule za Sekondari kujisomea.
“Tunaishikuru sana Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kutambua umuhimu wa elimu na kuona ulazima wa kutugawia vitabu hivi. Kwa binafsi ninaahidi kuvisimiamia na kuvitunza ili view msaada hata kwa vizazi vijavyo”, Alisema Mwalimu Kisimbo.
Naye Mwl. Sawe kaimu Mkuu wa Shule ya sekondari Rubeho alisema shule yake imepata jumla ya vitabu 483 vya masomo saba, vya masomo mbalimbali ikiwemo Kemia, Fizikia, Uraia, Hisabati, Baiyolojia, TEHAMA na Historia
“Kwa shule ya Sekondari Rubeho tumemokea junla ya vitabu 483 vya masomo saba tofauti tofauti ikiwepo Sayansi, Uraia, Hisabati na Jiografia. Vitabu hivi vitajenga msingi bora wa kujifunza kwa watoto wetu na watapata elimu vile ipasavyo”. Alifafanua Mwl. Sawe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa