Cosmas Mathias Njingo;
GAIRO.
Oktoba 8, 2022.
Halmashauri imepokea fedha jumla ya Shilingi 669,367,943.00 (Milioni Mia sita Sitini na Tisa, laki tatu sitini na Saba Elfu, mia tisa arobaini na tatu, bila senti) za utekelzaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo sekta ya Elimu, kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Ujenzi wa vyumba 2 (40,000,000) vya madarasa shule ya sekondari Kibedya
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Msifwaki Haule, katika mazungumzo yake na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Bw. Cosmas Mathias Njingo, ofisini kwake Oktoba 8. 2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bi Msifwaki Haule
“Halmashauri yetu ni miongoni mwa Halmashauri zilizopokea fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo sekta ya Elimu Sekondari. Kwa upande wetu, tumepata kiasi chi Shilingi 669,367,943 kwa jili ya ujenzi wa vyumba 22 vya madarasa na nyumba 4 (pacha mbili) kwa ajili ya walimu.
Mradi ya ujenzi wa nyumba pacha (2/1) ya Walimu Shule ya Sekondari Majembwe kata ya Msingisi
Bi. Msifwaki alisema; kati ya fedha hizo, Shilingi 440,000, 000 (Milioni mia nne na arobaini) zinaelekezwa kwenye ujezi wa vyumba 22 vya madarasa katika shule za Sekondari 7, pamoja na ununuzi wa samani za ndani, ikiwepo viti 1,100 na meza 1,100, kwa lengo la kupuguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa ili kuwezesha wanafunzi watakaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kuwa katika mazingira bora na rafiki ya kujifunzia.
Kaimu Mkurugenzi huyo alitaja Shule za Sekondari zilizonufaika na mgawo wa fedha hizo za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kuwa ni pamoja na; Gairo Sekondari (07) Tsh. 140,000,000, A.M. Shabbiby (01) Tsh.20, 000,000, Rubeho (02) Tsh. 40, 000,000, Kibedya (02) Tsh.40 000,000. Iyogwe (03) Tsh. 60, 000,000, Nongwe (02) Tsh. 40, 000,000, Chakwale Chigage (05) Tsh. 100, 000,000
Ujenzi wa chumba kimoja cha Darasa shule ya Sekondari A.M. Shabbiby
Kuhusu ujenzi wa nyumba za Walimu, Bi. Msifwaki alisema; Shilingi milioni 229,367,943 (milioni miambili ishirini na tisa, laki tatu na sitini na saba elfu, miatisa arobaini na tatu) zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba nne (04) pacha, ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuhakikisha inaboresha mazingira ya utendaji kazi kwa walimu, kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa nyumba bora za makazi, hali iliyowalazimu kuishi umbali mrefu na vituo vya vya kazi, hivyo kupunguza ari ya kufundisha na kusababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Majengo 3 vya vyumba 7 vya madarasa shule ya sekodari Gairo (Sh.140,000,000)
Hadi sasa zoezi la usafishaji wa maeneo, upimaji ramani na uchimbaji wa msingi wa majengo husika umekamilika kwa baadhi ya maeneo, huku mafundi wa kufyatua tofali wakiendelea na shughuili ya kuzalisha tofali tayari kuanza kwa kazi za ujenzi, ambapo hadi kufikia Disemba 10.2022, Halmashauri inatarajia kukabidhi majengo yote, kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa, yakiwa yamekamilika na Samani zake zote za ndani.
Kwa upande mwingine Bi. Haule ametoa rai kwa Wananchi waliopo kwenye maeneo yanayotekelezwa miradi hiyo, kila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha anashiriki katika kusimamia na kulinda vifaa vyote vya ujenzi ili kuzuia vitendo vya kihalifu ikiwepo wizi wa vifaa hivyo, na kwamba kwa kufanya hivyo watawezesha miradi hiyo kutekelezwa katika viwango na ubora unaotakiwa.
Na kuongeza kuwa ubora wa miundombinu hiyo uendane na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na Serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mradi wa ujenzi wa Vyumba 2 (40,000,000) vya madarasa Rubeho Sekondari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa