• Mawasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
GAIRO DISTRICT COUNCIL
GAIRO DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Authorities Halmashauri ya Wilaya ya Gairo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Halmashauri
    • Dira
    • Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Divisheni za Halmashauri
      • Seksheni ya Rasilimali Watu
      • Seksheni ya Utawala
    • Divisheni ya Mipango na Ufuatiliaji
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Baraza la Madiwani
  • Miradi
    • Miradi ya Maendeleo
      • Sekta ya Elimu Msingi
        • Miradi Mipya
        • Miradi iliyokamilika
      • Sekta ya Elimu Sekondari
      • Sekta ya Afya
      • Sekta ya Barabara/Miundombinu
      • Sekta ya Maji
  • Machapisho
    • Katiba ya JMT
    • Sheria ndogo ndogo za Halmashauri
    • Hotuba Mbalimbali
    • Sera ya Elimu
    • Taarifa za Hesabu za Mwisho
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video

TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAIPONGEZA HALMASHAURI KWA MAANDALIZI MAZURI

Posted on: February 23rd, 2025

Na. Cosmas Njingo; GAIRO

Februari 23.2025

Maafisa kutoka Idara ya Habari na Elimu kwa Umma ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kwa hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika maandalizi ya zoezi la uandikishaji wapiga kura wapya pamoja na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Pongezi hizo zilitolewa Februari 21.2025, wakati wa ziara ya maafisa hao wilayani Gairo kwa ajili ya kufuatilia hatua za maandalizi zinazoendelea kabla ya kuanza rasmi kwa zoezi hilo muhimu la kitaifa.

Wakizungumza na watendaji wa halmashauri pamoja na wadau wa uchaguzi, maafisa hao walionesha kuridhishwa na namna ambavyo Gairo imejipanga katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uboreshaji wa daftari hilo.

"Ni dhahiri kuwa Gairo imechukua hatua makini za maandalizi, ikiwemo utoaji wa elimu kwa umma, maandalizi ya miundombinu na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali. Hii inaonesha dhamira ya dhati ya kuhakikisha kila mwenye sifa anashiriki kwenye zoezi hili," alisema mmoja wa maafisa wa NEC.

Kwa upande wao , viongozi wa Halmashauri ya Gairo wamesema wapo tayari kushirikiana na NEC pamoja na taasisi nyingine kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa.Zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari linatarajiwa kuwa chachu ya kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye uchaguzi mkuu ujao, huku NEC ikiendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.


Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWEYE USAILI WAOMBAJI NAFASI ZA AJIRA MTENDAJI WA KIJIJI III NA DEREVA II September 21, 2024
  • TANGAZO LA HALMASHAURI KUKUSANYA USHURU WA USAFI May 07, 2024
  • TANGAZO LA KUJIUNGA NA PROGRAM YA BBT May 18, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MAAFISA WATENDAJI WA VIJIJI NA DEREVA July 12, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • VIONGOZI WA DINI WAASWA KUSHIRIKIANA NA NEC KUHAMASISHA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    February 24, 2025
  • TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI YAIPONGEZA HALMASHAURI KWA MAANDALIZI MAZURI

    February 23, 2025
  • VYAMA VYA SISA VYAHIMIZWA KUHAMASISHA WANACHAMA WAO KUJITOKEZA KUSHIRIKI KATIKA AWAMU YA KWANZA YA UANDIKISHAJI, UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

    February 21, 2025
  • MKOA WA MOROGORO WAJIPANGA KUIWEKA WILAYA YA GAIRO KWENYE RAMANI YA UZALISHAJI WA PARACHICHI NCHINI

    February 19, 2025
  • Tazama zote

Video

WANAFUNZI DARASA LA SABA WAASWA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Zabuni za Manunuzi
  • Zabuni za Ujenzi
  • Huduma

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Tanzania
  • GAIRO ONLINE TV
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Mawasiliana nasi

    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.

    Sanduku la Posta: 40, GAIRO

    Simu ya Mezani: +255 787730665

    Simu ya Kiganjani: +255 717222572

    Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa