Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amewataka Wamiliki wa Shule Binafsi, shule za Umma, Walimu na Wadau wote wa Elimu Nchini kuacha kutumia shule kuendekeza vitendo vya Wizi na udanganyifu wakati wa mitihani ya Taifa.
Ametoa rai hiyo Februari 20.2023, Jijini Mwanza alipokutana na baadhi ya Wazazi wa Wanafunzi waliofutiwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kuhitimu Kidato cha nne 2022 kufuatia kubainika kwa vitendo vya udanganyifu wakati wa mitihani hiyo.
“Wazizi wenzangu poleni sana kwa yaliyotokea, nimekuja hapa kwa ajili ya kutoa ufafanunuzi wa mambo yaliyotokea dhidi ya wanafunzi ambao wamekamatwa wakifanya vitendo vya udanganyifu wakati wa mitihani. Naomba ieleweke kwamba udanganyifu na wizi wa mitihani unamadhara makubwa sana katika Nchi yetu” alisema Mhe. Prof. Mkenda.
Alisema kuwa shule zikitumika kuendekeza vitendo vya udanganyifu na wizi wa Mitihani Taifa linapata madhara makubwa matutu ikiwepo ukosefu wa haki, ukosefu wa maadili na ukosefu weledi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kitaalumu miongoni mwa vijana wanaohitimu masomo yao nabaadae kupata nyadhifa mbalimbali kwenye taasisi za umma na binasi.
“Tunafundishwa misikitini na makanisani kutenda haki na kutokudanya kwani vitendo vya namna hiyo vinasababisha wengine kukosa haki. Mfano anayeonyeshwa Mtihani na ambaye hajaonyeshwa wakati wa uchaguzi tunawanyima haki wale ambao hawajaona mitihani” alieleza Prof. Mkenda.
Alisema kumekuwepo na matukio ya baadhi ya majengo binafsi na umma kuporomoka, madaraja kubomoka na matumizi mabaya ya fedha za Umma kutokana na ukosefu wa maadili katika jamii unaosababishwa na tabia za wizi ambazo vijana wanajifunzia wakiwa shuleni.
“Nchi ya Tanzania inasimamia haki na Maadili lakini inapokuja swala la namna hiyo nchi inazalisha wasomi wasio na uadilifu kwa kuwa walianza kujifunza vitendo vya wizi na ukosefu wa maadili kuanzia shuleni”. Alifafanua.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa