Na Cosmas M. Njingo. GAIRO
Aprili 22.2023
UFAFANUZI TUHUMA ZA UBADHILIFU WA SH. MIL 100 ZA MIKOPO YA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU. *Naweka kumbukumbu sawa kuhusu Mil 100 za fedha za Mikopo ya Vijana, Wanawake na Watu Wenye Ulemavu.*
Nimekuwa nikiona taarifa mbalimbali zikitolewa na kuandikwa na baadhi ya Watu kwamba Kuna fedha milioni 100 za vikundi zimeliwa na Watumishi wa Halmashauri. Hili taarifa si sahihi, ni upotoshaji.
Usahihi wa taarifa ni kwamba, Timu ya Uchunguzi iliyoundwa na Mnamo Mwezi Februari 2023, ililenga kufanya Ufuatiliaji wa Mikopo ya Vikundi kupitia Mapato ya ndani. Lengo letu lilikuwa kutaka kujiridhisha kama fedha zinatolewa kwa walengwa, tija ya mikopo hiyo kwa maana uendelevu wa miradi na kuboreka kwa maisha ya wakopaji, urejeshaji wa mikopo kadhalika na uzingatiaji wa Kanuni na mwongozo wa Utoaji wa mikopo……
Kamati ilibaini changamoto kadhaa ikiwemo tabia ya baadhi ya Wananchi wanaonufaika na mikopo hiyo kutorejesha kabisa mikopo ambapo katika kipindi Cha Miaka 3 takribani kiasi Cha shilingi mil 100 hazijarejeshwa na Vikundi), baadhi ya vikundi kugawana mikopo bila kufanya miradi iliyokusudiwa na Vikundi kusambaratika, kutolewa kwa mikopo kwa Vikundi visivyokidhi vigezo, tija ndogo ya mikopo hiyo na baadhi ya mikopo kutolewa bila kuzingatia Mwongozo……
Kufautia dosari hizo, imeelekezwa kwamba;-
*Moja, ndani ya siku 14 Halmashauri ije na Mpango wa kurejesha fedha kutoka kwenye vikundi kwa maana ya Mkakati wa namna ya kuzifuatilia fedha hizo kutoka kwa waliokopeswa, siyo Halmashauri irejeshe fedha ndani ya siku 14 kama baadhi ya Watu wanavyopotosha.*
*Pili, TAKUKURU wanaendelea na ufuatiliaji. Kama Kuna Mtumishi au Mwananchi amehusika katika jambo lolote la Rushwa hatua za kisheria zitachukuliwa.*
Hivyo, fedha Shilingi mil 100 zilizozungumzwa ni fedha za Mikopo ambazo Vikundi havijarejesha kwa Halmashauri.
Ikumbukwe kwamba, baadhi ya wakopaji ni ndugu zetu, wananchi wenzetu, Vijana wenzetu hivyo na wao wanahusika, na niwaombe tuwajulishe kwamba fedha hizo lazima zirejeshwe ili wananchi wengine wanufaike pindi Serikali itakapotoa utaratibu mpya. Hatutasita kuchukua hatua kwa wale waliochukua fedha za Halmashauri bila kurejesha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa