Na. Cosmas Mathias Njingo;GAIRO
Juni 9.2023
TZS.1,400,000,000 (1.4 Bil) KUTEKELEZA AWAMU YA KWANZA YA UJENZI WA CHUO CHA MAFUNZO YA UFUNDI STADI GAIRO
#Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame amezindua rasmi utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Chuo Cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Wilaya ya Gairo, ambao utasaidia kuongeza fursa kwa vijana kupata ujuzi wa kujiajiri wao wenyewe baada ya kuhitimu masomo.
Tukio hilo la Uzinduzi limefanyika Mei.7.2023 kwenye Kijiji Cha Msingisi Kata ya Msingisi Wilayani Gairo ambapo chuo hicho kitajengwa.
Kwa mujibu wa Mthibiti Mkuu wa Ubora wa Elimu Wilayani Gairo Bi. Tatu Samizi, hadi kukamilika kwa awamu ya kwanza ya Ujenzi wa Majengo tisa, jumla ya Shingi Bilioni Moja, na milioni mianne zitatumika , na kufafanua kuwa tayari kiasi Cha shilingi 228 Milioni kimeshawekwa kwenye akaunti kwa ajili ya kuanza utekelezaji.
"Mhe. Mgeni Rasmi awamu ya kwanza ya Mradi huu inajumuisha Ujenzi wa Majengo 9, likiwepo Jengo la Utawala, Jengo la Mlizi, Jengo la Kuzalishia Umeme (power house), Utawala, Nyumba ya Mkuu wa Chuo, Ofisi, Jengo la vyumba 03 vya madarasa, na kiasi cha shilingi Bilioni Moja na milioni mianne zitatumika katika Ujenzi wa Majengo hayo tisa". Alifafanua Bi. Samizi.
Akihutubia Wakazi wa eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Makame alisema kwa mwaka huu wa 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imepokea fedha zaidi ya Bilioni mbili kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya Elimu ya Awali na Msingi ili kuongeza utoaji wa huduma na kuweka Mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia, hivyo uwepo wa chuo hicho cha VETA Wilayani Gairo ni fursa ya kipekee kwa Wakazi wa Gairo.
"Mhe. Rais ameleta Fedha nyingi sana kwenye Wilaya yetu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali sekta ya Elimu, afya, barabara na maji. Na sasa tumepokea fedha shilingi Bilioni Moja nukata nne za ujenzi wa Chuo cha VETA, hii ni fursa kwa vijana wetu kupata ujuzi utakao wasaidia kujiajiri". Alisema Mhe. Makame.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo Ndg. Danistani Mwendi alisema maendeleo ya kasi yanayotokea Wilayani humo, ni juhudi kubwa za Mhe. Shabiby Mbunge wa Jimbo la Gairo ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania upatikanaji wa Fedha kutoka serikali kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa