Na. Cosmas Mathias Njingo
GAIRO, MOROGOR
Oktoba 15.2022
Ukoseefu wa Mahakama yenye uwezo wa kushughulikia kesi za makosa ya Ubakaji na ulawiti kumechangia kupunguza kasi ya kushughulikia mashauri ya vitendo vya ukatili wa kijinsia Wilayani Gairo.
Hii inatokana na umbali mrefu wa kufuata huduma za kimahakama katika Wilaya ya Kilosa zaidi ya Umbali wa Kilometa 130 kutoka Gairo.
Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Jeshi la Polisi Wilayani Gairo la Jinsia, Mkaguzi wa Jeshi hilo, Insp. Hope amesema hali ya umaskini imesababisha kesi nyingi kushindwa kuendelea kutokana na Waathirika wa vitendo vya Ulawiti na Ubakaji kushindwa kugharamia gharama za Usafiri na pesa za kujikimu wakati wa kuhudhuria kesi Mahakamani kutokana na uwezo wao wa kipato kuwa mdogo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa