Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Taasisis ya Chakula na Lishe Tanzania inaendesha utafiti wa Kitaifa kwa lengo la kubaini hali ya Lishe nchini. Utafiti huu umeanza mwezi Septemba na unatarajia kukamilika Novemba 2018, ukitumia methodolojia iitwayo “ SMART” ikiwa na maana ya ukusanyaji wa Takwimu na Uchambuzi wake kwa wakati na kuchukua hatua stahiki ili kutatua matatizo yaliyopo kwa sasa na kuandaa mazingira ya kujikinga na matatizo hayo.
Utafiti huu ni wa pili kufanyika Kitaifa kwani wa kwanza ulifanyika mwaka 2014.Utafiti huu unafanyika katika Mikao yote 26 ya Tanzania bara na Mikoa 5 ya Zanzibar. Sampuli ya kaya zinachaguliwa kushiriki kwa kufuata utaratibu maalumu wa kitaaluma ili kuweza kuziwakilisha kaya nyingine.
Walengwa katika utafiti huu ni Watoto chini ya miaka mitano ambao wanapimwa uzito, urefu na mzingo wa mkono. Walengwa wengine ni Wanawake walioko kwenye umri wa kuzaa (15-49) ambapo wanapimwa uzito, urefu na wingi wa damu na wanawake wajawazito wanapimwa mzingo wa mkono.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo utafiti huu unaanza tarehe 18-20 /10/2018 katika Kata ya Mkalama Mitaa ya Songe, Kwibobodo na Misheni, Kata ya Italagwe Kijiji cha Ijava kitongoji cha Chang’ombe na Ngutoto, Kata ya Magoweko mtaa wa Magoweko.
Hivyo watafiti wanapopita katika maeneo hayo wananchi mnaombwa kuwapa ushirikiano
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa