Cosmas Mathias Njingo;
MOROGORO.
Oktoba 4, 2022.
Pamoja na kuwepo kwa wastani mzuri wa mvua kwa mwaka, mabonde ya maji, ardhi yenye rutuba inayostawisha mazao ya aina mbalimbali mkoani Morogoro, uzalishaji wa mazao ya kilimo bado ni hafifu ikilinganishwa na mikoa mingine.
Uhafifu wa uzalishji wa mazo hayo unaelezwa unachangiwa na kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwepo ukosefu wa elimu ya matumizi bora ya ardhi, kilimo kisichozingatia kanuni bora za kilimo, migogoro ya wakulima na Wafugani pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani, hususani usafiri ili kuwafikia Wanachi kwa urahisi na kwa Wakati.
Inaelezwa kuwa uzalishaji wa zao la mahindi ni wastani wa tani 1.5 badala ya tani 6 kwa ekari moja, Mpunga unazalishwa wastani wa tani 2.3 badala ya tani 6 kwa ekari moja,viazi tani 2.6 bada;a ya tani 20, wakati uzalishji wa zao la ndizi ni wastani wa tani 4.4 badala ya tani 35.5 kwa ekari moja.
Sababu nyingine zinazotajwa kuchangia uzalishaji hafifu ni pamoja na matumizi ya mbegu za kienyeji, kilimo cha kutegemea mvua, matumiz ya mbolea isiyo sahihi au kutotumia kabisa mbolea, kutokujua hali ya udongo na aina ya mazai unaostawisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa