GAIRO,
Shirika la Mviwamoro linatokeleza mradi wa SET limetoa mafunzo kwa vijana 50 wa Wilaya ya Gairo.mafunzo hayo yamehusisha nadharia na vitendo katika mapishi ya vyakula mbali mbali ili kuwawezesha kuwa wa jasiriamali watakaojikwamua kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja
Aidha baada ya mafunzo hayo vijana hao wamepatiwa vifaa vya kuanza ujasiriamali wa kupika chakula kwa kupewa vitendea kazi kama meza,viti,vyombo,friji,mafuta,sukari,mmafuta kama vianzio katika kuanza kutekeleza biashara hizo sambamba na kulipiwa kodi katika maeneo ya kufanyia ujasiliamali huo wa kupika chakula.
Katika mafunzo hayo vijana hao wamepata elimu namna ya kuweza kusajili vikundi vyao na pamoja na kujiwekea akiba kwa kuwa na vikoba ambapo vikundi viwili vimetengenezwa na wame patiwa elimu namna ya kuweka akiba zao pamoja na vifaa kama sanduku,vitabu na leja ya vikundi.
Vijana walio nufaika 50, wameunda vikundi 8 vyenye idadi ya watu wa 5 pamoja na wajasiriamali wasionavikundi 7
Mradi huu umelenga kumuinua kijana kiuchumi na kumfanya kijana mmoja mmoja kuweza kujitegemea na kuendesha maisha yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa