GAIRO, MOROGORO.
Na. Cosmas Mathias Njingo.
AGOSTI 23.2022
Katika kuhakikisha Watanzania wanapata elimu ya kutosha kuhusu utunzajia, uhifadhi wa mazingira na upandaji miti, ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi yanayosababishwa na hali ya ukame, Waendesha Baiskeli wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamefanya matembezi ya hiari kutumia baiskeli wakiwa na lengo la kuendeleza jitihada za Serikali na Wadau wengine za kampeni ya upandaji miti.
(Kitalu cha Miti kilicho oteshwa na vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa ziara yao mwaka 2021 katika shule ya Sekondari Sekwao Wilaya ya Gairo)
Vijana hao wapatao 30 kutoka Nchi saba (07) za Afrika Mashariki wameshikiri kwenye shughuli mbalimbali za uhifadhi wa mazingira, ikiwepo upandaji wa miti na umwagiliaji maji wa kitalu cha miti katika shule ya Sekondari Sekwao Kata ya Ukwamani Wilaya ya Gairo.
Akizungumza baada ya kukamilisha zoezi la upandaji wa Miti, mmoja wa Viongozi wa Vijana hao alisema swala la utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti ni jambo la kila Mwananchi, hivyo ni wajibu kuhakikisha miti inapandwa kwa wingi katika maeneo ya Taasisi, Makazi na sehembu mbalimbali za shughuli za Kijamii.
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rachel Nyangasi (Mwenye kofia ya njano) wakishiriki katika zaozi la upandaji miti pamoja na Vijana wa Jumuiya ya Afrika mashariki, wakati wa ziara ya vijana hao Agosti 20.2022)
“Ni muhimu kwa kila Mtanzania kuwa balozi mzuri katika kuhamasisha shughuli za utunzaji na uhifadhi wa Mazingira. Ni muhimu sana katika kulinda uoto wa asili, lakini pia ni mojawapo ya mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na Mabadiliko ya Tabia Nchi”. Alisema Kiongozi huyo.
Hivi karibuni Wilaya ya Gairo ilifanya kampeni kubwa ya Urithi wa Kijani iliyo ongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, ambapo miti zaidi ya laki sita (600,000) ilipandwa katika maeneo mbalimbali ya Mji wa gairo ikiwepo Taasisi za Umma, meneo ya Makazi na kando kando ya Barabara kuu ya Morogoro Dodoma.
(Diwani wa Kata ya Ukwamani Mhe. Frank Mbaigwa (mwenye fulana nyeupe) akimwagilia kitalu cha miche ya miti pamoja na baadhi ya wananchi)
Akizungumza na Vijana hao waendesha Baiskeli Mhe. Makame aliwapongeza Waendesha basikeli hao kwa kushiriki kuendeleza zoezi la kampeni ya urithi wa kijani, ushiriki wao katika zoezi la upandaji wa miti na kumwagilia maji katika vitalu vya miche ya miti ambavyo Vijana hao waliviotesha wenyewe wakati wa matembezi yao mwaka 2021.
(Mkuu wa msafara wa Vijana wa EAC akitoa maelekezo ya upandaji wa miti)
“Kwa niaba ya Wananchi wenzangu wa Wilaya ya Gairo, ninachukua nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru kwa kushiriki kwenye kampeni ya urithi wa kijani. Tumefarijika sana na uzalendo wenu. Lakini pia msichoke kuendeleza kampeni ya upandaji miti katika mikoa mingine mtakayopita.
(Baadhi ya Wananchi, Vijana wa Skauti pamoja na Viongozi wakipata maelekezo kuhusu zoezi la upandaji wa Miti)
Sambamba na hayo Mhe. Makame akawaomba vijana hao kuendelea kuhamasisha swala la Utalii na vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki ikiwepo Kutangaza mbuga za wanyama, Hifadhi za Taifa na Mlima Kilimanjaro ambao umwekuwa na historia kubwa kwa nch za Kenya na Tanzania.
Vijana wa EAC wakimwagilia maji kwenye vitalu vya miche ya miti shule ya Sekondari Sekwao)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa