Na. Cosmas Mathias Njingo.
GAIRO, Morogoro.
Oktoba 25.2022
Imeelezwa kuwa, uwepo wa vikundi vya kiuchumi vya akiba na mikopo vya wanawake wanufaika wa TASAF, imekuwa ni chachu katika kuogeza kasi ya uchangia na utekelezaji wa shughuli za maendeloe, na kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi kuanzia ngazi ya famila na jamii nzima kwa ujumla, kwa Wananchi wa Kijiji cha Ikwamba Kata ya Mandege Wilayani Gairo.
Hayo yamebainishwa na Viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, katika mahojiano maalum na Mwandishi wetu, wakati wakitoa maoni yao kuhusu mchango wa Vikundi vya akiba na mikopo, vya kiuchumi hususani wanufaika wa TASAF, katika kuongeza kasi ya maendeleo kijijini hapo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ikwamba, Bwn. Yosia Yoram, na Afisa Mtendaji wa Kjiji hicho (mwenye shati la kijani) katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Kikundi cha Kiuchumi cha Upendo, kinajojishughulisha na ufugaji wa Kuku wa Kienyeji (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
Akitoa maoni yake Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ikwamba Bwn. Yosia Adrian Yoram, alisema kijiji hicho kimepiga hatua kubwa kimandeleo kwa kipindi cha mize saba tisa iliyopita, tangu kuanzishwa kwa vikundi vya Kiuchumi vya Wanawake, chini ya mpango wa TASAF, ikilinganishwa na hapo awali kasi ya maendeleo ilikuwa ni ndogo sana kutokana na uwezo mdogo wa kuiuchumi hali iliyosababisha ushiriki wa wanawake kwenye kuchangia maendelo kuwa wa kiwango kidogo.
“Kwakweli nipende kuishukuru Serikali yetu, imefanya kazi kubwa ya kuwainua Wanawake hapa kijijni kwetu Kupitia wao kasi ya maendeleo imeogezeka kwani ushiriki wa Wanawake umekuwa mkubwa, na wamekuwa wakijitolea kifedha na nguvu zao katika shughuli zote zinazohusu maendeleo ya kijiji chetu”. Alisifia Mweyekiti huyo wa Serikali ya Kijiji.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ikwamba, Bwn. Yosia Yoram, na Afisa Mtendaji wa Kjiji hicho, Bwn. Kashidye S. Kassote (mwenye shati la kijani) katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Kikundi cha Kiuchumi cha JITAHIDI kinajojishughulisha na bishara ya mahindi (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO).
Mwenyekiti Yoram akaeleza kuwa mwanamke ana mchango mkubwa katika kuinua pato la taifa endapo atashirikishwa kikamilifu katika kufanya maamuzi, japokuwa swala usawa baina ya wanawake na wanaume bado inakwepwa na wanajamii waliowengi.
Figure 1Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ikwamba, Bwn. Yosia Yoram, na Afisa Mtendaji wa Kjiji hicho, Bwn. Kashidye S. Kassote (mwenye shati la kijani) katika picha ya Pamoja na Viongozi wa Kikundi cha Kiuchumi cha AMANI kinajojishughulisha na bishara ya maharage (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO).
Kwa upande wake Afisa Mtedaji wa kijiji hicho Bwn. Kashindye Severine Kassote, amesema kijiji cha ikwamba kina mabadiliko chanya kimaendeleo na kiuchumi kutokana na hamasa kubwa inayofanywa na wanavikundi hivyo katika kuhimiza na kushiriki moja kwa moja kwenye maendelo ya kijiji hicho
“Tungu kuundwa kwa vikundi hivi hapa kijijini, sisi viongozi tunatembea kwa kujivunia uwepo wao kwani tunaona kuna mabadiliko makubwa sana, na matokeo chanya katika uhamsishaji, uchangiaji na ushiriki wa Wananchi kwenye shughuli za maendeleo. Kwa ufupi, \kijiji cha Ikwamba kimepiga hatua kubwa sana kiuchumi ikilinganishwa na hapo awali kabla ya kuanzishwa vikundi hivi” Alifafanua Mtendaji huyo.
Bwn. Kassote akaeleza Zaidi kuwa Kijiji cha Ikwamba kina jumla ya vikundi 11, kati ya hivyo 6 vipo kwenye mpango wa TASAF, huku vitano bado ninaendelea na taratibu za kukamilisha maelekezo mbalimbali ili viweze kuingizwa katika mpango huo, hali aliyosema itaharakisha Zaidi upatikanaji wa maeneleo kwa mwana kikundi mmoja mmoja na kijiji kizima kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa