Na. Cosmas Mathias Njingo.GAIRO, MOROGORO.
AGOSTI 22.2022
Vijana waendesha Baiskeli wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamewaomba Viongozi wa Jumuiya hiyo kuendelea kudumisha amani upendo na Mshikamano baina ya nchi hizo ili kufugua fursa mbalimbali kwa vijana, wanafunzi na Wafanya biashara, sambamba na kusaidia kupatikana kwa amani katika Mataifa ya DRC Congo na Sudani Kusini, ambayo yamekumbwa na machafuko ya ndani kwa ndani kwa kipindi kirefu.
(Mmoja awa Viongozi w waendesha Baiskeli kutoka Jumuiya ya Afrika kashariki akuzungumza kuhusu ziara yao ya matembezi ya baiskeli kuzunguka Nchi Wanachama wa EAC)
Wametoa kauli hiyo Agost 20.2022 Wilayani Gairo wakati wa ziara yao kuelekea mkoa Dodoma wakitokea, Mombasa Nchini Kenya ambako walianzia mbio hizo, Safari yao ikilenga kuingia Nchi za Rwanda, Burudi, Kongo DRC, Uganda kupitia Tanzania na baadae kuhitimisha mbio hizo za Baiskeli Jijini Nairobi Nchini Kenya.
“Sisi vijana waendesha Baiskeli kutoka Nchi zilizopo kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki, wito wetu kwa viongozi wa Nchi zote Wanachama wa Jumuiya hii, waendelee kuimarisha amani na kuepuka machafuko ambayo yanahatarisha usalama wa maisha ya Wananchi wao na kutishia kuvunjika kwa Jumuiya hii endapo amani itakosekana katika Mataifa yetu”. Alisema Mmoja wa Viongozi wa Vijana hao.
(Vijana wa Jumuiya ya EAC walipotembelea Wilaya Gairo wakati wa ziara ya matembezi ya baiskeli kuzunguka Nchi Wananacha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki)
Alisema ni muhimu kuilinda Tunu ya amani iliyopo ambayo iliasisiwa na Viongozi wanao itakia mema Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwani kwa kufanya hivyo fursa mbalimbali zitafunguka na kuwezesha vijana kunufaika kupitia Biashara, ajira, michezo na fursa nyingine za kuwaunganisha Wananchi na kaimarisha mahusiano.
Wakitokea Mkoani Morogoro na kupiga Kambi katika Wilaya ya Gairo ambapo walifanya shuguli mbali mbali ikiwepo Hamasa ya Sensa ya Watu na Makazi Upandaji wa Miti, Vijana hao wamesema wanafurahishwa na namna ambavyo Serikali ya Tanzania ilivyo imarisha ulinzi na usalama hali ambayo imewafanya Wananchi wake kuwa na amani ya kutosha na kuendesha shughuli za kiuchumu kwa uhuru pasipo na machafuko ya aina yoyote.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame aliwapongeza vijana hao kwa moyo wao wa uzalendo wa kujitolea kutembea kwa basikeli kwenye Mataifa ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kueneza jumbe mbalimbali ikiwepo swala la kudumisha amani, upandaji miti na utunzaji wa mazingira pamoja na maswala ya Utalii.
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Jabiri Omari Makame akizungumza na Vijana kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa ziara ya Viajana hao Wilayani Gairo, Agosti 20.2022)
“Niwapongeze vijana wenzetu kwa uzalendo mkubwa mlio uonyesha, mmeamua kutembea kwa kutumia Baiskeli mkizunguka nchi zote saba, kwa lengo la kuhamsisha Mataifa haya kuimarisha amani na mshikamo, lakini pia kutukumbusha kuendelea kutunza mazingira”. Alisema Mhe. Makame.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Racgel Nyangasi, aliwashukuru vijana hao kwa hamasa waliyoitoa na kukubali kwao kupeperusha bendera ya Sensa katika mikoa yote watakayo pita kuelekea nchi za Congo DRC, Rwanda na Burudi, ambapo aliwazadia kiasi cha Shilingi laki moja kwa ajili ya mahitaji madogo madogo ya njiani.
(Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rachel Nyangasi akikabidhi fedha kiasi cha Sh.100,000 (laki moja) za kuwezesha vijana hao kupata maji ya kunywa njiani)
“Kwa niaba ya Halmashauri, nachukua fursa hii kuwapongeza vijana wetu kwa ujasiri mkubwa ambao wameuonyesha, lakini kitendo cha kukubali kutembea na Bendera ya Sensa ni jambo kubwa la sana tunatakiwa kuwatia moyo. Hivyo basi ninawapa kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya maji ya kunywa njiani”. Alisema Mhe. Nyangasi.
Agosti 20.2022 Wilaya ya Gairo ilipokea Timu ya Vijana hao wakitokea Mji wa Mombasa Nchini Kenya katika ziara yao ya kuhamsisha Viongozi wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kudumisha Amani, Umoja, Mshikamano, Utunzaji wa Mazingira na upandaji wa Miti, wakizungukia Nchi zote za EAU.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa