Cosmas Mathias Njingo;
GAIRO, Morogoro
Septemba 27, 2022.
Rai imetolewa kwa Viongozi wa dini Wilayani Gairo, kuwaeleza ukweli waumini wao juu ya athari za vitendo vya ukatili wa kinsia ambavyo vimeshika hatamu kwa kasi kubwa hali ambayo inatishia ustawi wa family
Rai hiyo imetolewa na Viongozi wa Jukwaa la Amani Wilaya ya Gairo wakati wa Warsha ya siku mmoja iliyoendeshwa na Asasi ya Kiraia ya Pelum Tanzania kupitia mradi wa Woman Rural Cultivating Change (RWCC), iliyofanyika katika ukumbi mdogo wa Mikutano wa Halmashauri Septemba 27.2022
Mwenyekiti Mwenza wa Jukwaa la Amani Gairo Mchungaji Canon Benedict Mbelwa (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo:GAIRO)
“Lazima sisi viongozi wa dini tuongee na waumini wetu na kuwaleza ukweli kuhusu ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea. Bila kusema ukweli ukatili utaendelea kuongezeka”. Alisema Mchungaji Canon Mbelwa.
Canon Mbelwa ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Jukwaa la Amani Gairo alisema endapo jamii haitaelezwa ukweli kuhusu athari za matendo ya ukatili huo, kundi linalo athirika zaidi ni kundi la watoto hali inayoweza kuwaathirika kisaikolojia na kuporomosha maenendeleo yao kitaaluma.
“Tusipo sema ukweli kwa waumini wetu kuhusu hili tatizo, watakaoathirika zaidi ni watoto, wanapoona matukio ya aina hii yakifanywa na wazazi wao, yanawatoa kwenye mfumo bora wa maisha, wanaharibika kisaikolojia, napengine vitendo vya ukatili vikachochea kushusha uwezo wao kitaaluma mashuleni”. Alifafanua Mchungaji Mbelwa.
Kwa upande wake Kiongozi wa Jumuiya ya Wazee Wilayani Humo Mwalimu Mstaafu Mama Lesso, alisema kuongezeka kwa vitendo vya ukatili katika jamii kunatokana na kuporomoka kwa maadili kunakosababishwa na kukosekana hofu ya Mungu hali ambayo amesema imewafanya watu wengu kuwa na roho zisizo za kibinadamu.
“Hofu ya Mungu katika kizazi cha leo haipo kabisa, binadamu tumegeuka kuwa na tabia za kinyama, hakuna huruma. Unakuta mtu anafanya matendo ambayo si yakibinadamu anamtendea mwenzake matendo ya kinyama. Hii inatokana na upendo kupungua ndiyo maana hata Hofu ya Mungu haiopo Mioyoni mwao”. Alibainisha mama Lesso.
Awali akiwasilisha mada kuhusu madahara ya Ukatili wa Kijinsia Muwezeshaji wa warsha hiyo kutoka Asasi ya Pelum, chini ya Mradi wa RWCC, Afisa Program na Mafunzo Bi.Anna Marwa, alisema ipo haja ya viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu na kufanya maombi mazito ili ibadilike na kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
“Viongozi wa dini bado mnakazi kubwa sana, msichoke kukemea, kufundisha na kufanya maombi ya nguvu, kuombea familia zetu hasa wanaume ili hofu ya Mungu itawale. Viongozi wa Dini mna nafasi kubwa sana katika kukemea jambo hili.”Alisitiza.
Bi. Marwa akafafanua kuwa vitendo vya ukatili ni hali ya mtu kumtendea mtu mwingine jambo baya kinyume na makubaliano ama kinyume na maandiko Matakatifu ya Dini na kinyume cha Katiba na Sheria za Nchi.
Muwezeshaji wa warsha hiyo, Bi.Anna Marwa Afisa Program na Mafunzo kutoka Asasi ya Pelum, chini ya Mradi wa RWCC akiwasilisha mada kuhusu ukatili wa kijinisia (Picha Na. Cosmas Njingo-GAIRO)
Afisa Progamu huyo huyo alitaja baadhi ya citendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoripotiwa kukithiri katika jamii ni pamoja na Ukatili wa Kingono, lugha chafu dhidi ya wanawake na Watoto, udhalilishji, ukeketaji, mashambulio ya mwili na matendo yanayofanana na hayo.
Warsha hiyo ya siku 1 iliwakutanisha wadau mbalimbali ikiwepo Viongozi wa Dini, Wataalam kutoka halmashauri kupitia Idara ya Elimu Msingi na Sekondari, Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Wawakilishi wa Wazee na baadhi ya Waelimishaji wa kupinga maswala ya ukatili wa kijinsia ngazi za vijiji kutoka kata za Rugeho na Chagongwe.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku moja ya kupinga ukatili wa kijinsia chini ya Mradi wa RWCC (Picha Na. Cosmas Mathias Njingo-GAIRO)
PELUM Tanzania chini ya mradi wa RWCC imepanga kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za kilimo, kutoa elimu kwa jamii ili kutambua wajibu, haki na usawa wa Kijinsia, kutoa fursa kwa Wanawake kuweza kushiriki kwenye nafasiz za uongozi sambamba na kumuwezesha mwanamake kutambua nafasi yake katika kufanya maamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa