Cosmas Mathias Njingo;
MOROGORO.
Oktoba 2, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa, amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Wataalam wa Kilimo wa Mkoa huo, kuhakikisha wanahimiza wakulima kujiandikisha katika daftari la wakulima, ili kunufaika na punguzo la bei ya mbolea za ruzuku.
Ametoa wito huo Oktoba Mosi 2022, katika kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Kilimo Marathoni, kilichofanyika kwenye viwanja vya Jamhuri Manispaa ya Morogoro, ambapo alisema ni wajibu wa viongozi wote kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha na kuhimiza wakulima kujiandikishwa kwenye daftari hilo ili kuiwezesha Serikali kutambua idadi yao, hali ambayo itarahisisha kuwahudumia.
Mhe. Fatma Mwassa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akifungua kikao cha Wadau wa Kilimo kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena Manispaa ya Morogoro.
“Jambo kubwa kwa sasa tuhimize wakulima kujisajili, kwani kupitia zoezi hili wakulima watapata fursa mbalimbali ikiwepo kunufaika na punguzo la bei za bembejeo za kilimo, kwa kuwa mama yetu Mhe. Samia Suluhu Hassan ameonyesha mapenzi makubwa kwa wakulima wetu kwa kuwashusia bei ya mbolea na Mbegu kutokana na ruzuku aliyoilekeza kwa Wakulima”. Alisisitiza Mhe. Mwassa.
Mkuu huyo wa Mkoa akasme kuwa, Mkoa wa Morogoro una Wakulima wasiopungua 470,000 (laki nne na elfu sabini), lakini wakulima waliojiandikisha ni asilimia 33 tu ya wakulima wote, hivyo ni vyema Wataalam wa Kilimo kwa ngazi zote kuhakikisha wanawafikia wakulima wote na kuwapa elimu kuhusu umuhimu wa kusajiliwa katika daftari la kudumu la Wakulima, ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo iliyokusudia katika kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija nchini.
Baadi ya wadau walioshikiri mbio za umbali mbali mbali baada ya kukabidhiwa tuzo zao na Mhe. Fatma Mwassa, katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa
“Mkoa wetu unakadiriwa kuwa na Wakulima laki nne na sabini elfu, lakini hadi sasa ni asilimia 33 tu ya wakulima wote walioandishwa. Bado hali ya uandikishaji hairidhishi, hivyo nendeni mkawahimize wakulima wetu wapata kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya Wakulima ili kutimiza malengo ya Serikali ya kuwahudumia wakulika wote kwa lengo la kukifanya kilimo kuwa na tija kwa mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa kwa ujumla”, Alielekeza Mkuu wa Mkoa Mhe. Mwassa.
Hitimisho la Wiki ya Mbio za Kilimo (Kilimo Marathon) Mkoa wa Morogoro liilitangu na kikao kazi cha wadau wa kilimo kilimo kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Morena Hotel chini ya Mhe. Mwassa kujadili changamoto na mikakati mbalimbali ya kuinua sekta ya kilimo pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Baadhi ya wahiriki wa Kilimo Marathoni wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fatma Mwassa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Pamoja na shughuli nyingine kilimo marathon iliambatana na maonesho ya bidaa mbalimbali za mazao ya kilimo, pembejeo na mbolea za ruzuku pamoja na teknolijia mbalimbali za kisas zinazotumika katika mapinduzi ya kisekta ili kuongeza tija kwenye shughuli za kilimo na ufugaji.
Washiriki wa maoneho ya Kilimo Marathoni kutoka kikundi cha Chinyankala saa
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa