Na. Cosmas Njingo. GAIRO
Mei 29/2024.
Rai imetolewa kwa viongozi Wilayani Gairo kushirikikwenye mchakato mzima wa uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga kura sambamba na kutoa elimu kwa Umma kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika kati ya mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa Mei 25.2024 na Mhe. Jabiri makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo alipokuwa akizingumza na Viongozi ngazi za Kata wakati wa kikao cha Baraza la Wazi la taarifa za Januari-Machi 2023/2024, uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
“Tunaelekea kwenye mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, wajibu wetu Viongozi ni kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa zoezi hili, lakini pia twendeni tukatoe elimu kwa Wananchi wetu kuhusu uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao mwaka huu tutatekeleza shughuli hiyo”. Mkuu wa Wilaya aliweaambia viongozi hao
Makame alisema pamoja na kutoa elimu kwa umma pia viongozi hao wanahimizwa kuhamasishana kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi huo kwani kila mmoja anayo haki kikatiba ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Aidha Mhe. Makame akaonya kuwa uchaguzi ni miongoni mwa mambo matano yanayowakilisha taswira ya Nchi, na kwamba hayapaswi kufanyiwa masikhara na mtu yoyote. Kwani yeyote atakaye leta masikhara au kuonesha nia ovu ya kuhujumu zoezi la uchaguzi atakuwa amejitumbukiza kwenye mkondo wa sheria yeye mwenyewe.
“Uchaguzi ni miongoni mwa mambo matano ambayo hatupaswi kuyafanyia masikhara kwa namna yoyote ile au kuchezea kwa namna yoyote ile. Haitakiwi kucheza na Uchaguzi Mkuu, ni jambo nyeti sana”. Alitaja
Menginge alitaja kuwa ni pamoja namitihani yote ya kitaifa, kuanzia darasa la nne, Darasa la saba kwa Shule za Msingi, Kidato cha pili na Nne kwa shule za Sekondari, Mwenge wa Uhuru na ziara za Viongozi wakuu wa Kitaita Unaposikia mitihani ya Kitaifa, ni jambo nyeti sana .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa