Tanzania – Mei 2025
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jimbo la Gairo, imevihimiza vyama vya siasa nchini kuhakikisha vinahamasisha wanachama na wafuasi wao kujitokeza kwa wingi kushiriki katika awamu ya kwanza ya uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ikiwa ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Wito huo umetolewa na Afisa Mwandikishaji Msaidizi wa Tume katika Jimbo la gairo Bi Jane Sanga, katika kikao kazi na viongozi wa vyama vya Siasa Wilaya ya Gairo, kilichoketi Februari 21. 2025, kuelekea uzinduzi rasmi wa zoezi hilo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe hadi 7 machi 12025 katika maeneo mbalimbali ya nchi, ambapo wananchi wanahamasishwa kujisajili kwa mara ya kwanza au kuboresha taarifa zao zilizopo katika daftari hilo.
Akizungumza na Viongozi hao, Bi. Jane Sanga alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vyama vya siasa katika mchakato huo kwa kuwa wao ni wadau wakuu wa uchaguzi na wana nafasi kubwa katika kuhakikisha wananchi wanatimiza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.
"Vyama vya siasa vina jukumu la msingi kuhakikisha wanachama wao wanapata elimu ya uchaguzi, wanajitokeza katika vituo vya kujiandikisha na kuhakikisha taarifa zao ziko sahihi. Hili ni zoezi la kitaifa na la kidemokrasia ambalo linahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Tume, vyama vya siasa na wananchi," alisema msemaji huyo.
Aidha, NEC imewataka viongozi wa vyama kuwaelimisha wanachama kuhusu umuhimu wa ushiriki katika uandikishaji huo kama njia ya kujiandaa kushiriki kikamilifu kwenye chaguzi zijazo, huku ikikumbusha kuwa daftari hilo ndilo linalotumika rasmi kwenye uchaguzi wowote wa kitaifa au wa serikali za mitaa.
Wananchi wote wanaostahili kuandikishwa, wakiwemo vijana waliotimiza umri wa miaka 18 au wanaotarajia kutimiza umri huo kabla ya uchaguzi, wametakiwa kujitokeza na kufika kwenye vituo vilivyotengwa kwa ajili ya huduma hiyo.
Uandikishaji na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni hatua muhimu inayochangia uhalali na uwazi wa mchakato wa uchaguzi nchini, na hivyo ushiriki wa kila mwananchi na taasisi husika unahitajika kwa mafanikio ya demokrasia ya Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa