Na. Cosmas Mathias Njingo. DAR ES SALAAM
Juni 19.2024
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaasa Waandishi wa Habari na Wadau wa Sekta ya Habari nchini kutumia taaluma zao vizuri kwa ufanya uchambuzi wa habari, kutoa taarifa sahihi kwa umma na kuisema vizuri Serikali badala ya kuandika mapungufu pekee ya Serikali.
Ametoa wito huo Juni 18.2024 akifungua kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari katika ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, ambalo Wadau wa sekata ya Habari watakutana kwa siku mbili hadi Juni 19.2024 kujadili mafanikio ya sekta hiyo, changamoto na mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma za habari na mawasiliano Nchini.
“Nitoe rai yangu kwa Waandishi wa habari Nchini kote, mjitahidi kuandika mazuri na kuisemea vizuri Nchi yetu ya Tanzania, badala ya kuandika habari za kuichafua Serikali. Ninyi ni watu muhimu sana wa kutangaza yaliyomema ambayo yanaleta tija kwa Wananachi”. Alisema Mhe. Rais Samia.
Samia aliwaambia Washiriki wa Kongamano hilo kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari chanya kwa jamii pamoja na kukanusha taarifa mbalimbali za upotoshaji zinazosambazwa na baadhi ya Waandishi wasio zingatia maadili ya Taaluma hiyo, huku wengine wakiitukana Serikali katika uso wa dunia, hali ambayo alisema inalenga kuzua taharuki na kuharibu taswira njema ya Nchi kwenye nyanja za Kimataifa.
“Tumieni vizuri kalamu zenu kuhabarisha Umma yale mema ambayo Serikali inayafanya, tunamiradi mingi ya maendeleo inatekelezwa huko kwenye ngazi za Halmashauri, wajulisheini Wananchi kuhusu miradi hiyo. Lakini cha ajabu ukiingia huko kwenye mitandao ya kijamii unakutana na matusi tu ya kuichafua Serikali”. Alisikitishwa.
Aidha Mhe. Rais Samia aliwataka Wanahabari hao kufanya uchambuzi wa kina wa taarifa kabla ya kuzirusha kwa jamii ili kupata usahihi wa kile wanachokusudia kuuhabarisha Umma, na hiyo itasaidia Wanachi kupata taarifa za kina, badala ya kusikia jambo na kulirusha bila kufanya uchambuzi wa kutosha.
Kongamano hilo la Maendeleo ya Sekta ya Habari limehuduhriwa na Washiriki mbalimbali kutoka Wizara na Taasisi za Umma, Binafsi, Viongozi wa Vyombo vya Habari, Waandishi wa Habari, Maafisa Habari, Uhusiano na Itifaki wa Serikali na Wadau wengine, ambapo litafuatiwa na Kikaoa kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali kuanzia Juni 20 hadi 22.2022
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa