Na, Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Sekta ya Madini imatajwa kuwa chanzo muhimu cha kukuza uchumi na kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani ya Nachi na kwamba kupitia makusanyo yanayotokana na fursa za uwekezaji katika sekta hii serikali imeweza kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati sambamba na kuimarisha miundombinu mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame alipotembelea mgodi wa dhahabu wa Kitaita kata ya Leshata na kufanya mazungumzo na wachimbaji wadogowadogo mgodini hapo Mei 15 2022. Ambapo kabla ya kuongea na wachimbaji hao Mhe. Makame alijionea shughuli mbali mbali za kiuchumi zinazoendelea kwenye eneo hilo.
“Madini ni vyanzo muhimu vya mapato ambavyo tunavitegemea kwenye Taifa letu. Wilaya yetu ya Gairo uwepo wa haya madini kutasaidia tupate mapato kutoka kwa wachimbaji wenyewe, lakini pia tupate mapato kutoka kwa wajasiliamali ambao wanafanya shughuli zao hapa, lakini pia tupate mapato kutoka kwa mawakala wanao nunua na kuuza madni”. Alisema Mhe. Makame.
Akaongeza kuwa “Mapato haya ya Serikali ndiyo ambayo tunayatumia kujenga shule, ili kuwasomesha watoto wetu, kuboresha miundombinu ya Maji, Umeme na Barabara sambamba na kutatua changamoto mbalimbali”.
Mkuu huyo wa Wilaya akawataka Viongozi, wachimbaji hao na wajasiliamali wote wanao endesha shughuli zao za kiuchumi katika mgodi huo kuhakikisha kila mmoja anakuwa balozi mwema katika kulipa mapato ya Serikali bila kukwepa.
“Tuwe wazalendo wa kulipa kodi na mapato ya Selikali, kila mmoja wetu anatakiwa kuwa balozi wa kusimamia hili lakini ukulipa kodi au ushuru hakikisha umepata risiti. Viongozi wote mlioko hapa na ninyi wote mkiona kuna viashiria vyovyote vya ukwepaji kulipa kodi za Serikali toeni taarifa kwa viongozi ili hatua stahiki zichukuliwe”, alisisitiza Mhe. Makame.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya akatumia fursa hiyo kuwa asa Wanabchi waliopo katika eneo hilo kuchukua tahadgari za kutosha katika kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya kuambukiza kama vile UKIMWI, magonjwa ya zinaa na malaria pamoja na magonjwa ya milipuko ikiwepo kipindupindu ili kulinda afya zao zisidhurike.
“Lakini ndugu zangu kwa wingi wenu huu ni muhimu sana kuchukua tahadhari ya kutosha kujikinga na Malaria, Magonjwa ya zina pia kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonja ya milipuko kama matumbo ya kuhara na kipindupindu”. Aliwakumbusha.
Mheshimiwa makame akawakumbusha wachimbaji wadogo wadogo hao kuhusu uchimbaji wa vyoo vya kutosha na kuizingatia matumizi sahihi kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa watu kujisaidia kwenye maeneo ambayo siyo rasmi na kwamba ni muhimu kila mmoja kuwa mlizi wa mwingine dhidi ya shughuli yoyote inayochafua mazingira hasa kujisaidia vichakani.
“Swala kutunza na kuhifadhi mazingira ni jambo muhimu sana, hivyo lazima mchimbe vyoo vya kutosham lakini kuwepo na matumzi sahihi ya vyo hivyo. Kila mmoja awe mlizi katika kutunza mazingira kwa kuhakikisha wanaochafua mazingira na kujisaidia vichakani wanachukuliwa hatia ikiwepo kutozwa faini”. Alisema Makeme.
Katika mkutano huo Mkuu huyo wa Wilaya akawakumbusha Wananchi na wachimbaji wadogo wagodo kuhusu swala la usalama wa eneo hilo ambapo alisisitiza kuwa kila mtu anaye ingia katika mgodi huo lazima aripoti kwa uongozi wa mgodi na kusajili ili atambalike.
“Kila anayeingia hapa ni lazima alipoti kwenye ofisi za viongozi wa eneo hili ajiandikishe tumtambue kwa majina yake anatokea wapi na shughuli anayo kuja kuifanya ikiwezekana aonyeshe kitambulisho chake alicho nacho hii itasaidia kuepusha madhara yoyote ya kiulinzi na usalama”. alisema.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Gairo Mheshimiwa Jabiri Omari Makame aliambatana na Mwneyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Ndugu Shabani Sajilo, Katibu wa CCM Wilaya Bi. Highness Munisi, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rachel Nyangasi, Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Susan Nyanda, Wajumbe wa KUU Wilaya, Afisa Madini Wilaya ndugu Maira pamoja na wakuu wa idara na vitengo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa