Wilaya ya Gairo imezindua mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia sekta ya Elimu ikiwa ni kampeni ya kuboresha miundombinu chakavu mashuleni sambamba na kupambana na utoro uliokithiri na mimba za utotoni ambavyo vinatajwa kuchangia udumavu wa elimu kwa shule za msingi.
Uzinduzi huo umefanyika Januari 14.2022 katika Ukumbi wa Nazareth kata ya Magoweko chini ya Mhe. Jabiri Omari Makame, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, umeenda sambamba na harambee ya kuchangia fedha za kutunisha Mfuko wa Elimu kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya elimu.
“Jumla ya Shilingi 38,630,000 zimepatikana kwa muda mfupi sana. Nianze kwa kuwashukuru wadau wote mlio onyesha nia ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya wamau ya sita za kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele ili vijana wetu wasome katika mazingira safi na rafiki”, alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Na kuongeza kuwa “Ikiwa ni mara ya kwanza kwa Wilaya yetu kuendesha zoezi hili, nina kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa fedha hizi kwa kukubali kwenu kuniunga mkono katika kampeni hii muhimu ya kusaidia kutatua changamoto zinazo wakabili watoto wetu mashuleni”, alifafanua.
Akitangaza kiasi kilichopatikana katika changizo hilo Mhe. Makame aliwapongeza Wadau hao kwa kuonyesha nia ya dhati kunusuru sekta ya elimu, kwani jukumu la kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu mashuleni ni la jamii nzima ambapo aliwaomba wadau hao kuendelea kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hasan katika hushughulikia kero za elimu.
Akasema kwamba “ Swala la ujenzo wa elimu bora siyo swala la walimu peke yao bali jamii nzima inawajibika kuhakikisha inashiriki katika kuboresha hali ya taaluma kuanzia nyumbani hadi mashuleni ili kutokomeza utoro, mimba za utotoni na utendaji kazi mbovu wa walimu kwa kuhakikisha miundombinu yote ya elimu ni safi, salana na rafiki”.
Uchakavu wa miundombinu, ubovu wa majengo ya shule, upungufu wa madarasa, madawati, viti na meza pamoja na upungufu wa walimu ni kati ya sababu zinazotajwa kuwa kikwazo kikubwa za kupunguza ari ya kujifunza na kufundisha na kwamba zimechochea matokeo mabovu katika mitihani ya kujipima na Taifa.
Kiasi cha Shilingi milioni 38,630,000 zilipatikana wakati wa zoezi la harambee ya kutunisha mfuko huo ambapo kati ya hizo Shilingi 40,000 ni fedha tasilimu na ahadi shilingi 38,590,000 huku wakala wa misitu gairo (TFS) pamoja na Mhifadhi wa Milima ya Ukaguru walichangia kiasi cha shilingi 20,000,000.
Kuanzishwa kwa Mfuko kunalenga kusaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo ikabili sekta ya Elimu ambazo zinatajwa kuwa kikwazo kikubwa cha kuzorotesha ustawi wa elimu ngazi ya Msingi na Sekondari.
Baadhi ya Wadau wakitoa maoni yao kuhusu kuimarisha Sekta ya elimu walishauri fedha zilizopatikana kupitia harambee hiyo zielekezewe kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ya Wasichana yenye mchepuo wa Sayansi ili kuzalisha wanasayansi wengi wanawake.
“Mimi ninashauri mfuko huu ukishaa anzishwa, fedha zinakazo patikana Uongozi wa Wilaya uone namna ya kuwekeza kwenye ujenzi wa shule ya wasichana ya sayansi”, alishauri mmoja wa wadau hao ambae jina lake halikuweza kupatikana.
Aidha kupitia harambee hiyo Wakala wa Misitu (TFS) Gairo kwa kushirikiana na Mhifadhi Milima ya Ukaguru walitoa jumla ya Shilingi 20,000,000 ambazo walisema zitaelekezwa kwenye kuboresha miundombinu chakavu shule ya msingi mandenge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa