(Mhe. Anthony Peter Mavunde. Naibu Waziri wa Kilimo)
Na. Cosmas mathias Njingo. GAIRO DC
Ingawa Sekta za Kilimo na Mifugo zinatajwa kuwa na mchango mkubwa katika kuinua pato na Uchumi wa Taifa kwa kiasi kikubwa, mabadiliko ya Tabia nchi yameleta changamoto nyingi kwa wakulima na wafugaji ikipweo kuzalisha mazao na mifugo kwa ubora hafifu isiyoendana na mahitaji ya soko hivyo kushusa pato kwa mkulima na mmoja mmoja hususani wanaozalisha kwa kiwango kidogo ukilinganisha na wazalishaji wakubwa.
(Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Sekta za Kilimo na Mifugo Wilayani Gairo katika ukumbi wa Nazareth)
Kauli hiyo imetolewa na Mhe. Athony Peter Mavunde (MB) Naibu Waziri wa Kilimo pamoja na Mhe Abdallah Ulega (MB) Naibu wa ziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakakti wakitoa hotuba zao kwa njia ya Mtandao (Video Conference) kwenye Mkutano mkubwa wa Wadau wa Sekta hizo mbili uliofanyika katika ukumbi wa Nazareth Wilayani Gairo, Mkutano ambao uliitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Jabiri Omari Makame.
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame akifungua Mkutano wa Wadau wa Sekta za Kilimo za Mifugo katika ukumbi wa Nazareth Wilayani Gairo)
Mhe. Mavunde alisema sekta hizi zinagusa maisha ya Watanzania kwa kiwango kikubwa kwani zinachangia kutengeneza ajira na kupunguza umaskini hasa katika kundi la Vijana, nakuongeza kuwa kongama hilo lililo wakutanisha Wadau wa Sekta za Kilimo na Mifugo litaleta majawabu sahihi katika kushughulikia changamoto zinazowakabili Wakulima na Wafugaji, kwa wakati ambao Serikali kwa upande wake ikiendelea kutafuta namna bora wa kuwazesha wadau wa sekta hizi mbili kuendesha shughuli zao katika mazingira rafiki ili waweze kupiga hatia kiuchumi.
"Tunatanbua kilimo kinachangia sehemu kubwa ya mapato ya Nchi yetu, kinakuza ajira na kuinua vipato hasa kundi la vijana.Inagawa zipo changamoto nyingi ambazo kimsingi zimekuwa vikwazo katika kumwinua Mkulima na Mfugaji, mojawapo ni mabadiliko ya Tabia Nchi, upatikanaji wa Masoko ya uhakika, Uwezeshwaji katika upatikanaji wa pembejeo, elimu ya kilimo bora na mifugo pamoja na mikopo nafuu kwa wadau wa sekta hizi mbili", Alitaja Mhe. Naibu Waziri wa Kilimo.
(Afisa Kilimo Mwandamizi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Ntirankiza Misibo akiwasilisha mada ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa Wahiriki wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Kilimo na Mifugo, katika ukumbi wa Nazareth Wilayani Gairo)
Mhe. Naibu Waziri Mavunde alisema Serikali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishirikiana na Mhe. Isdory Mipango, Makamu wa Rais na Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mapoja wote watatu wameonyesha nia ya dhati na utashi wa kisiasa katika kuhakikisha Sekta hizi mbili zinapiga hatua kutatua changamoto zinazowakabili wakulima na Wafugaji pamoja na wadau wengine ili kupunguza Umaskini kwa Watanzania, na kuongeza kuwa Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 imatenga kiasi cha shilingi Milioni miatisa na hamsini na nne (954 Milioni) katika bajeti yake ikilinganishwa na Bajeti ya Shilingi milioni miambili tisini na nne (294 Milioni) kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2021/2022.
Alisema "Katika kudhihirisha hili kwa vitendo, Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishirikiana na Mhe. Isdory Mipango, Makamu wa Rais na Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mapoja wote watatu wameonyesha nia ya dhati na utashi wa kisiasa katika kuhakikisha Sekta hizi mbili zinaenda kutatua changamoto zinazo wakabili wakulima na wafugaji wetu ili kuwapunguzia Umaskini, na nwaka huu wa fedha wa 2022/2023 Bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kutoka shilingi Miambili tisini na Nne Milioni hadi kufikia Shilingi mia Tisa hamsini na nne milioni, utaona kuna ongezeko la zaidi ya shilingi mia sita Milioni katika baheti ya mwaka huu".
(Mhe shimiwa Abdallah, Naibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi)
Kwa upande wake Naibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. shimiwa Abdallah Ulega alisema Wizara yake kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023 kupitia Benki ya kilimo na Benki nyingine zinazo jihusisha na sekta za Kilimo na Mifugo, imajikita zaidi katika kuwawezesha wafugaji kupata mikopo nafuu ili kuwasaidia kuinua mitaji waweze kuedesha shughuli za ufugaji na kuongeza thamani katika mazao ya mifugo.
"Serikali kupitia Benki ya kilimo na Benki nyingine zinazo jihusisha na sekta za Kilimo na Mifugo imeamua kuwasidia wakulima hasa sekta binafsi kupata fursa ya mikopo nafuu kwa ajili ya wawezesha kuendesha shughuli za ufugaji katika mazingira rafiki, hii ni fursa muhimu hasa kwenye eneo la unenepeshaji wa Ng'ombe, Mbuzi na Kondoo, sambamba na kuongeza thamani ya mazao yatokanayo na mifugo lengo ikiwa ni kupanua wigo wa soko la ndani na ngazi za kimataifa". Alifafanua Mhe. Ulega.
(Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wadau wa Sekta za Kilimo na Mifugo Wilayani Gairo katika ukumbi wa Nazareth)
Mhe. Ulega amesema Wizara ya mifugo kwa kuwatumia maafisa ugani waliopo katika ngazi za kata na vijiji wilayani Gairo ipo tayari kutoa elimu juu ya unenepeshaji wa mifugo, upatikanaji wa malighafi za kuweza kusindika na kuchakata mazao yatokanayo na mifugo, umuhimu wa upatikanaji wa fursa za mikopo nafuu pamoja na namna bora ya uandishi wa maandiko ya kuomba mkopo kwenye Benki ya kilimo.
"Sisi ka Wizara tumejipanga vizuri na tumeamuwa kuwatumia maafisa ugani wa mifugo ngazi za Kata na Vijiji uwafikia wfugaji na kuwape elimu juu ya ufugaji bora na wakisasa wenye tija. Badala ya mfugaji kuwa na kundi kubwa la mifugo tutamuelimisha kuwa na kundi dogo lakini lenye tija, sambamba na kutoa elimu kuhusu namna bora ya unenepeshaji wa hiyo mifugo, uchakataji wa mazao ya mifugo, usindikaji na uhifadhi ili kukuza thamani na kuweza kupata soko la uhakika ndani ya Nchi na masoko ya Kimataifa". Alitanabahisha Naibu Waziri Ulega.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame akizungumzia athari za nabadiliko ya tabia Nchi alisema uzalishaji umepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na ukosefu wa mvua za uhakika hali iliyosababishwa na Wananchi kukaribu mazingira kwa kukata hovyo miti jivyo kusababisha hali ya jangwa inaweza kuleta ukame.
(Dr. Godbless Luhunga, Mkuu wa Idara ya Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, akiwasilisha mada ya hali ya mifugo Wilayani humo wakati wa Mkutano wa Wadau wa Sekta za Kilimo na Mifugo)
"Shughuli za kibinadamu za kujitafutia kipato hususani ukataji wa miti kwenye misitu na hifadhi za mapori kumechangia sana haya matokeo ya mabadiliko ya tabia Nchi tunayo yaona leo. Mifugo inaduma na kukonda kwa kukosa nyasi na maji lakini pia kilimo hakina tija kutokana na ukame unaosabishwa na tabia mbaya ya baadhi yetu ya kufyeka miti na kuharibi mazingira. Alisema Mhe. Jabiri
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Gairo wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa Mkutano wa Wadau wa Sekta za Kilimo na Mifugo)
(Afisa Habari, Mawasiliano na Uhusiani Bwana Cosmas Mathias Njingo (kushoto) na Bi Joyce Shinji Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Halmashauri ya Wilaya ya Gairo
wakifanya maandalizi ya urushaji wa mada mbalimbali kwa njia ya Teknolojia ya kisasa kupitia projekta)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa