Cosmas Mathias Njingo;
MOROGORO.
Oktoba 3, 2022.
Wadau wa Kilimo Mko wa Morogoro Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Fatma Abubakar Mwassa wamekutana katika kongamano la wadau wa Sekta hiyo kujadili changamoto na mikakati mbalimbali ya kilimo chenye tija bila kuleta athari za mazingira na kijamii.
Kongamano hilo la siku 1 limefanyika Septemba 28.2022 katika ukumbi wa Hoteli ya Morena iliyopo Msamvu Manisapaa ya Morogoro, ambapo wadau kutoka taasisi za Umma na Binafsi zinazojihusisha na tafiti na elimu ya kilimo walikutana pamoja na Wataala wa Idara za kilimo kutoka Halmashauri za Mkoa huo.
Akifungua kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Mwassa, alisema kongamano hilo ni muhimu kwa mustakabali wa afya ya sekta ya kilimo, kwani kunawawezesha wadau kuona fursa za kiuchumi zilizopo na kuzitumia, badala ya kutumia muda mwingi kulalamika au kutatua miogogoro.
“Ili Wananachi wa Mkoa wa Morogoro walime kwa tija, tunahitaji kufanya mabadiliko (transformation) ya kifikra, tunahitaji mabadiliko ya namna tunavyotenda mambo na mabadiliko ya kimfumo, na inapobidi mabadiliko ya kiuongozi. Hivyo kupitia kongamano hili ni imani yangu kuwa yale tutakayojadili yataleta changamoto katika kutumia fursa zilizopo ndani ya mkoa wetu, ili kilimo kiwe na tija kwa faida ya mtu mmoja mmoja, mkoa na Taifa kwa ujumla”. Alisema Mhe. Mwassa.
Alisema Mkoa wa morogoro una ardhi yenye rutuba ya kutosha na hali ya hewa nzuri inayostawisha mazao mengi, mvua za wasta kati ya 600mm hadi 800mm, lakini pamoja na hali hiyo bado sekta ya kilimo haifanyi vizuri.
Akizungumzia kuhusu migogoro ya Ardhi, Mhe. Mwassa alibainisha kuwa Morogoro ni miongoni mwa mikoa 5 nchini inayokabiliwa na migogoro sugu ya Ardhi, ikiwepo kati ya kijiji na kijiji, wakulima na wafugaji na katika ya koo flani na koo nyingine. Kwa kuongeza kuwa Watendaji wa Serikali wameshindwa kusimamia vizuri juu ya matumizi ya ardhi iliyopo.
“Bado tunaeneo kubwa sana ikilinganishwa na idadi ya watu waliopo mkoa wa Morogoro. Hivyo nisingependa kuona ongezeko la migogoro ya ardhi kati ya Wakulima na Wafugaji kama tuliyonayo hivi sasa.
Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa pili Tanzania kwa Ukubwa, ukiwa na hekta za mraba 73,039,000. Hadi kufikia mwaka 2012 Morogoro ilikadiriwa kuwa na wakaazi 2,827,281 (milioni mbili laki nane thamanini na saba elfu miambili themanini na moja), kwa mujibu wa sense ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 kukiwa kuna ongezeko la asilimia 3.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa