GAIRO, MOROGORO.
Na. Cosmas Mathias Njingo.
Wakati Tanzania ikiendelea na maandalizi mbalimbali ya kungia katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 20, Timu ya Vijana waendesha Baiskeli wapatao 35 kutoka Mataifa yanayounda umoja wa Jumuiya ya Afrika mashariki wameamua kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupeperusha Bendera ya Sensa kwa lengo la kutangaza ujumbe wa zoezi hilo na kuhamasisha Watanzania kushiriki kuhesabiwa kupitia matembezi ya basikeli kuzunguka Nchi zailizopo katika ukansa wa Afirika Mashariki.
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame (kulia), akikabidi Bendera ya Sensa kwa Kiongozi wa waendesha Baiskeli kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki)
Agosti 20.2022 Wilaya ya Gairo ilipokea Timu ya Vijana hao wakitokea Mji wa Mombasa Nchini Kenya katika ziara yao ya kuhamsisha Viongozi wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kudumisha Amani, Umoja, Mshikamano, Utunzaji wa Mazingira na upandaji wa Miti, wakipita kwenye Nchi zote za EAU.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame aliwakabidhi vijana hao Bendera ya Sensa na kuwataka kuendelea kutangaza ujumbe huo kwa kila mkoa wa Tanzania ambao wamepanga kupita kuelekea Nchi za Congo, Rwanda, Burudi, Sudani Kusini na Uganda kabla ya kuhitimisha matembezi hayo katika Jiji la Nairobi Nchini Kenya ili kuongeza hamasa na uelewa wa pamoja kwa wananchi watambue umuhimu wa kuhesabiwa.
(Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame akiongoza matembezi ya Waendesha Baiskeli kutoka Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki kuhamasisha amani, umoja, utunzaji wa mazingira na kueneza ujumbe wa Sensa ya watu na Makazi)
Mmoja wa Viongozi wa vijana hao waendesha Basikeli kutoka nchi zipatazo Saba (7) za Kumuiya ya Afrilka mashariki alisema Serikali haiwezi kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwa haitambui idadi ya watu wake, na kusisitiza kuwa ni muhimu kila mtanzania kujitokeza kuhesabiwa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu na kuharakisha maendeleo.
“Mipango ndiyo inayo endesha Nchi, inasaidia Serikali kubaini mahali flani kuwa watu kiasi Fulani na wanahitaji huduma flani, mfano Shule, mahitaji ya vituo vya kutolea huduma za afya, miundombinu ya barabara na uboreshaji wa huduma nyingine za kijamii.” alieleza kiongozi huyo.
(Waendesha Baiskeli kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki)
Naye Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, amewapongeza vijana hao kwa kazu nzuri ya kizalendo kwa kujitolea kutembea kwa Baiskeli kuzunguka katika Nchi zote za Jumuiya ya EAC kwa lengo la kutangaza Umoja na mshikamano, ambapo aliwataka kutumia fursa hiyo kutangaza ujumbe wa Sensa kwa Watanzania katika mikoa yote ya Tanzania Watakayopita.
“Ninawapongeza kwa kazi nzuri ya kizalendo, mmeonyesha ujasiri mkubwa wa kutembea kwa Baiskeli mkizunguka na ujumbe wa kueneza Amani, Mshikamano na Umoja. Nami ninawaomba kupitia matembezi haya mtusaidie kupeperusha Bendera yetu yenye ujumbe wa Sensa katika kila mkoa mtakao fika msisahau kuhamasisha kukushu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ili kila Mtanzania atambue umuhimu wa kuhesabiwa ifikapo Agosti 23.2022”. alisema Mhe. Makame.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa