Na.Cosmas Mathias Njingo, GAIRO
Agosti 17.2023
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame amewaasa Wahe. Madiwani, Wakuu wa Divisheni na Vitengo, Wataalam pamoja na watendaji wote wa Halmashauri kuimarisha upendo, kushirikiana, kufanya kazi kwa umoja huku kila mmoja akitambua nafasi yake katika kuwahudumia Wananchi kwani kwa kuunganisha umoja huo kunaimarisha nguvu katika kuwaletea maendelo Wananchi.
Makamame ametoa rai hiyo Agosti 11/2023 wakati wa kikao cha kawaida cha Baraza la Wahe. Madiwani kujadil taarifa za Robo ya Nne kwa kipindi cha Aprili Juni 2022/2023 kilichofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano wa Halmashauri.
“Mh. Mwenyekiti rai yangu kwa Waheshimiwa Madiwai wafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Watendaji wetu wa Kata, lakini pia kuhakikisha wanaimarisha umoja na kutambua vyema wajibu na nafasi ya kila mmoja katika kuwahudumia Wananchi; kwani Umoja wetu ndiyo nguvu yetu na silaya pekee ya kuwaletea Wananchi maendeleo”. Alisema Makame.
Kwa upande mwingine Mhe. Makame alipongeza juhudi za Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dakta Samia Suluhu Hassan; za kuimarisha na kuboresha huduma mbalibali kwa Wanachi wa Gairo, na kwamba mapinduzi ya kimaendeleo yanakuwa kwa kasi Wilayani humo.
“Naomba tumpigie makofi Rais wetu Dakta Samia Suluhu Hassan, kwa kweli anafanya kazi kubwa ya kutuletea maendeleo sisi wanagairo kwa kasi kubwa. Sisi sote ni mashahidi tumepokea fedha nyingi sana za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na mwaka huu mpya pia zimeingia fedha nyingine kwa ajili ya kumalizia miradi ilikwama na kuanza miradi mipya’. Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Makame alitaja sekta zzilizopokea fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali kuwa ni pamoja na Afya, Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, Kilimo, Mifugo na Uvuvi, sekta ya Barabara kupitia Wakala wa Barabara mjini na Vijijini (TARURA) miradi ya Umeme vijijini (REA) kupitia TANESCO pamoja na uchimbaji wa Visima vya maji na uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wa mabomba ya maji ili kuhakikisha Wananchi wa Gairo wananufaika na huduma bora za kijamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa