Cosmas Mathias Njingo;
MOROGORO.
Disemba 1.2022.
Diwani wa kata ya Leshata Mhe. Omary Mwende, amatoa rai kwa Wakazi wa Kata ya Leshata na kata nyingine za jirani kujenga utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara, ili kubaini hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kwani kwa kutambua hali zao kiafya kutawawezesha kujilinda na kuwalinda wengine dhini ya maambukizi hayo.
Mhe Omary Mwende, ametoa rai hiyo Disemba Mosi 2022, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambayo kiwilaya yalifanyika kwenye Kata hiyo ya Leshata na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwepo Mhe. Jabiri Omari Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo, ambayae alikuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Omari Makame (kulia), akiteta jambo na Mratibu wa UKIMWI (W) Mohamed Amri
“Leshata kwa sasa ni sehemu ya eneo lenye muingiliano mkubwa wa watu katika Wilaya ya Gairo, kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwepo uchimbaji wa madini. Watu wengi wamekusanyika hapa kujitafutia ridhiki kutoka maeneo mbalimbali ya Nchi yetu ya Tanzania. Rai yangu kwa Wananchi wenzangu wa kata ya Leshata na kata za jirani, tujitokeze kupima afya zetu ili tutambue hali ya maambukiz ya Virusi vya UKIMWI. Hii itatuwezesha kujilinda na kuwalinda wengine”. Alisema Mhe Mwende
Kawa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Makame alisema makakati wa serikali ni kufikia kiwango cha maambuikizi sifuri kufikia mwaka 2023, pasiwepo na mamabukizi mapya ya vizuri vya UKIMWI.
Mhe. Jabiri Omari Makame,Mkuu wa Wilaya ya Gairo
“Mpango wetu Serikali, ifikapo 2023 tunataka tufikie asilimia 95, 95, 95. Hii inamaanisha shabaha yetu ni kukomesha matukio ya unyanyapaa dhidi ya wanaoishi na maambukizi ya V.V.U kwa asilimia 95, tunalenga kuhakikisha kiwango cha unyanyapaa kifikie sifuri. Kusiwepo na Mtu hata mmoja kunyanyapaa mwingine au Mtu anayeishi na V.V.U kujinyanyapaa mwenyewe”. Alisema Mhe. Makame
Makame akataja mikakati mingine ni kupunguza vifo vinavyotokana na V.V.U kwa asilimi 95, sambamba na kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa asilimia 95. N akwamba lengo ikiwa ni kupata asilimi ‘0’ ya hali ya unyanyapaa, maambukizi mapya ya V.V.U na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo ifikapo 2030.
“Ili kuyafikia malengo hayo ndugu zangu, tunahitaji jitihada za pamoja kwa kushirikiana kati ya Serikali, Asasi za kiraia zinazojihusisha na mapambano dhidi ya V.V.U UKIMWI sambamba na Wadau wengine na mtu mmoja mmoja”. Alisema Mhe. Makame.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa