Na. Cosmas Mathiasn Njingo
Morogoro.
Septemba 30.2022
Pamoja na kuwepo kwa ardhi yenye rutuba nzuri zaidi ya hekari milioni mbili inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya biashara katika mkoa wa morogoro, ni asilimia 40 tu ya eneo la ardhi linalotumika kwa shughuli za kilimo, huku asilimia 60 zikibaki mapori tupu, hali ambayo inatajwa kuchangia uzalishaji usio na tija.
Dakta Chagoba Zaidi Mkangwa, Mtafiti Mstaafu kutoka Asasi ya Kiraia inayojihusisha na Utafiti, Ushauri na Taarifa za Kilimo, iliyopo Mkoani Morogoro, alisema pamoja na kuwepo na eneo kubwa la ardhi inayofaa kwa kilimo na ufugaji, ni sehemu ndogo tu ya ardhi inayotumika kwa ajili ya shughuli hizo, huku sehemu kubwa ya ardhi hiyo ikibaki bila matumizi yoyote, na kwamba Wakulima wengi hawajatambu namna ya kutumia fursa zilizopo.
“Tunaeneo kubwa sana la ardhi lenye ukubwa zaidi ya Hekari milioni mbili, lakini ni asilimia 40 tu inayotumika kwa ajili ya shughuli za kilimo, wakati asilimia 60 ya ardhi yote inabaki wazi. Lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa elimu juu ya matumizi ya fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo”. Alisema Dakta Mkamgwa.
Dakta Mkangwa, akasema kuwa Mkoa wa Morogoro una fursa nyingi za kwekeza katika sekta ya Kilimo, lakini wakazi wake wanakabiliwa na changamoto ukosefu wa elimu na taarifa za kutosha kuhusu namna ya kutumia fursa hizo ili kujikita katika kilimo chenye tija na kuondokana na hali ya umaskini.
“Pamoja na changanmoto mbalimbali, Wakazi wa Mkoa wa Morogor hawajui fursa nyingi zilizopo katika sekta ya kilimo, hii inasababisha kuwa na kilimo cha mazoea na matokea yake kupata mazao yasiyo na tija kwani chini ya asilimia 40 au chini ya hapo ya kiwango kinachotakiwa kuzalishwa”. Alisfafanua Daktari huyo.
Mkangwa akaeleza changamoto nyingine zinazosababisha kuzalisha mazao hafifu ni ukosefu wa elimu ya mbinu bora za kilimo, migogoro kati ya wakulima na wafugaji pamoja na uharibifu wa nazingira ikiwepo vyanzo vya maji na uchomaji wato misitu.
Aidha Dakta Mkangwa amewataka Wananchi hususani wakulima wa Mkoa wa Morogoro kutumia fursa hizo kwa kuhakikisha wanazingatia na kufuafuata kanuni za kilimo bora ili kuzalisha mazao yenye tija kwa lengo la kujikwamu kiuchumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa