Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amezindua mfumo wa Ruzuku za Pembejeo za Kilimo na Mbolea kwa Wakulima Nchini wenye thamani ya zaidi ya Shilingi mia moja na hamsini (150) za Kitanzania, pamoja na dola za Kimarekani Milioni sabini na saba (77) kwa ajili ya kuwapunguzia wakulima mzigo wa gharama za Pembejeo hususani Mbolea, kwa lengo la kuwawezesha kujikita katika kilimo chenye tija ili kukuza pato la mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
(Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya Sita, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
Akifunga hitimisho la Wiki la maadhimisho ya Maonesho ya shughuli za Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Agosti 8, 2022 Jijini Mbeya, Mhe. Rais amezitaka Wizara ya Fedha na Wizara ya Kilimo kuhakikisha Fedha za Ruzuku ya pembejeo za Kilimo zinawafikia wakulima kwa Wakati waweze kutimiza maelengo yao kuendana na misimu ya mvua.
“Natumia Fusra hii kuzitaka Wizara hizi mbili kuhakikisha Fedha za Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo zinapatikana na kuwafikia wakulima kwa Wakati kulingana na misimu” Aliagiza
Pia Mheshimiwa Rais akaziagiza Mamlaka za Serikali za mitaa nchini kuanzia ngazi za Mikoa, Wilaya, Kata vijiji na vitopngoji kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kusimamia usajili wa wakulima watakao nufaika na Ruzuku ya Pembejeo za kilimo.
“Ninawa agiza Viongozi wote ngazi za Mikoa, Wilaya, Kata na Vijiji kuhakikisha wanashiriki kusimamia usajili wa wakulima watakao nufaika na Ruzuku ya Pembejeo za kilimo.
Aidha amewataka wakulia wote kujisajili kwenye daftari la orodha ya Wakulima ili kuiwezesha Serekali kujua idadi yao kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma za ugani, upatikanaji wa pembejeo za Kilimo pamoja na fursa za mikopo ya wakulima na Wafugaji.
Kwa upande mwingi Rais Samia amaeigaza Wizara ya Kilimo ku
(Mhe. Hussein Bashe (MB), Waziri wa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji)
hakikisha Mifuko yote inayotumika kuhifadhia Mbolea iwekwe alama ya utambuzi, na kuzitaka kampuni zote zilizosajiliwa kusambaza mbolea nchini zinatangaza mawakala wao wa kuuza na kusambaza mbolea katika kila mkoa na Wilaya ili kuwawezesha Wananchi kutambua huduma zinapatikana kwa wakala yupi.
Pia Mhe. Rais, amewataka Wakuli, Wafugaji na Wavuvi kutumia elimu na ujuzi kupitia mafunzo waliyoyapata kwa kipindi chote cha maonesho hayo kwa kuzingatia mbinu bora za kilimo, ufugaji na uvuvi, na matumizi ya teknolojia mpya ili kuleta tija katika shughuli zao, kuongeza uzalishaji wa uhakika wa mazao kwa ajili ya chakula na biashara, sambamba na kujikwamua kiuchumi kwa ujumla.
“Wito wangu kwa wakulima, Wafugaji na Wavuvi, ni kutumia elimu na ujuzi, maarifa pamoja na teknolojia walizojifunza kwa kipindi chote cha Maonesho, kulete mapinduzi katika sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, ili kukidhi mahitaji ya Viwanda, pamoja na kutumia fursa hii adhimu ya upatikanaji wa taarifa muhimu za Masoko ya ndani na Nje ya nchi”. Alisisitiza Mhe. Samia.
Mhe. Rais Samia, amewezesha upatikanaji wa Pembejeo za Kilimo na Mbolea kwa bei nafuu ikilinganishwa na bei ya awali ambayo wakulima wengi wamekuwa wakilalamika kutokana na kupatikana kwa gharama kubwa hali iliyodaiwa kupunguza uzalishaji kwani wakulima wengi walijikita kwenye kilimo cha kati kukwepa gharama za mbolea na pembejeo.
Wizara ya Kilimo imetengewa kiasi cha Shilingi Milioni milioni mia tisa na hamsini (950) kwa ajili ya kuwezesha wakulima kukabiliana na changomto mbalimbali ambapo kati ya hizo Shilingi Milioni mia nne (400) zimeelekezwa katika kujenga na kuboresha miundombinu ya skimu za umwagiliaji nchini ili kufikia agenda ya 10/30 ya Kilimo ni Biashara.
(Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (MB), Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi)
Awali akitoa salamu kwa Mheshimiwa Rais mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo, Mhe. Dakta Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha, Mipango na Uchumi, alisema Serikali imeanaza kutilia mkazo na kuongeza nguvu zaidi kwenye sekta za uzalishaji ikiwepo Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, kasi ndogo ya kupanda kwa pato la mtu mmoja mmoja, sambamba na kuongeza kasi ya kupunguza umaskini.
“Mhe. Rais uliitisha kikao kilichojumisha Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Wizara za kisekta ambapo ulitueleza unakerwa na Kasi ndogo ya kupungua kwa umaskini, lakini pia ulitueleza namna ambavyo unakerwa na Ongezeko la ukosefu wa Ajira hususani kwa vijana, na ulisikitishwa sana na kiwango kidogo cha kupanda kwa pato la mtu mmoja mmoja”. Alisema Waziri Mwigulu.
Waziri Mwigulu alisema Mahitaji ya Bajeti yanaongezeka kuliko kasi ya Ukusanyaji wa mapato hali ambayo inaonyesha kuwepo kwa matumizi makubwa kuliko fedha zinazokusanywa, na kwamba changamoto hiyo inasababisha kasi ya kupunguza umaskini kwa Wananchi kuwa ndogo tofauti na matarajio ya Watanzania wengi.
Ili kukabiliana na changamoto hizo Mhe. Nchemba alisema Serikali imeongeza majeti katika Wizara ya Kilimo kutoka Shilingi Milioni 254 hadi shilingi milioni 950, kadhalika na Sekta nyingine za uzalishaji ikiwepo Ufugaji na Uvuvi zimetengewa Sh.268 bilioni, pamoja na Biashara nayo zimeongezewa bajeti kwa mwaka huu wa fedha 2022/2023.
Aidha Mhe. Nchemba alitoa rai kwa Watanzania kumsaidia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza bajeti hiyo kwa vitendo, ili wizara zote za kisekta zipate tija katika shughuli za uzalisha na kuzalisha ajira ili kuongeza pato laTaifa.
“Bajeti peke yake haiwezi ikafanya kazi na kuleta matunda katika maendeleo, fedha peke yake haiwezi ikaleta matunda katika maisha yetu, ni lazima kila Mtanzania kwa nafasi yake afanye kazi katika kutekeleza bajeti hii ili kila mmoja apate manufaa kwa mustakabali wa kukuza pato la mkulima mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”. Alisistiza Mhe. Waziri wa Fedha.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa alimwambia Mhe. Samia kuwa Wizara ya Tamisemi imajipanga vizuri kuhakikisha inatekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuwakomboa Wananchi kupitia sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ili kuhakikisha matarajio hayo yanafikiwa kwa asilimia 100.
(Mhe. Innocent Bashungwa (MB) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI)
“Mhe. Raisi, kilimo kimeshika hatamu, lakini wa kukishikisha hatamu ni Ofisi ya Rais Tamisemi Wizara ambao ninaiongoza Mimi. Nikuahidi tu kuwa, Mimi pamoja na Watumishi wenzangu upande wa Wizara, Wahe. Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, hatutakuwa tayari kukuangusha katika dhamira yako ya kuendelea kuleta mageuzi makubwa ya Wakuliam wetu Nchini, tutasimamia hili kwa vitendo”. Alisema Mhe. Bashungwa.
Maadhimisho haya ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi mwaka huu Kitaifa yamefanyika Jijini Mbeya, yakibebwa na kauli mbiu ya “Ajenda 10/30 isemayo Kilimo ni Biashara ambapo Agosti 1 2022 Mhe. Isdory Mipango alishiriki ufunguzi wake na Kufungwa Rasmi Agosti 8 2022 na Mhe. Samia Suluhu Hassa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(Mhe. Mashimba Ndaki (MB), Waziri wa Mifugo na Uvuvi)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa