Na Cosmas Mathias Ningo. 88 MOROGORO
Agosti 11.2023
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Seleman Jaffo amesema wakulima wanatakiwa kupewa elimu wafikapo katika Maonesho ya Nanenane kuhusu zao la Mchiki kusudu ni kuongeza uzalishaji wenye tija ili kuondia tatizo la mafuta hapa nchini.
Mhe. Jaffo amesema hayo Agosti 7, 2023 wakati akitembelea mabanda ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ili kuona teknolojia na shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji na Uvuvi zinavyofanyika.
Mhe. Adam Malima ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro amesema zao hilo hutoa mafuta mengi ikiwemo koli (mikungu) 20 hutoa Lita 5 za mafuta ya kupikia lakini wakulima wengi hutoa koli (mikungu) 20 kwa lita 1, hivyo amemtaka mmoja wa mtaalam wa kilimo cha michikichi kutoa elimu hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa