Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Juni 24.2024.
Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Gairo Bi. Shariafa Nabalang’anya, amewaasa Wakuu wa Divhisheni na Vitengo pamoja na Watendaji wengine wa Halmashauri kuwekeza katika Kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwepo parachichi na tumbaku, ili watakapo staafu wawe nashughuli mbadala ya kufanya.
Ametoa hamasa wakati wa kikao cha Wadau wa kilimo cha zao Tumbaku ya kukaushwa kwa jua kilichofanyika Juni 24.2024 katika ukumbi wa Mikutano wa Mkuu wa Wilaya, ambacho kiliwakutanisha Wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwepo Wakulima, Eataalam wa Kilimo na Wanunuzi wa Tumbaku kutoka taasisi ya Mkwawa ya Mjini Iringa.
“Hata sisi Wataalam, tutumie fursa hii kununua mashamba na kuwekeza kwenye Kilimo cha zao la Tumbaku, tusione kuwa kilimo ni cha Wananchi peke yao. Hivyo natumia nafasi hii kuwahamasisha Wakuu wa Divisheni na Vitengo kuona fursa zilizopo kwenye Kilimo”. Alisema Mkurugenzi huyo.
Sambamba na hayo pia amewasisitiza wataala hao kujiunga na vyama vya ushirika vya Wakulima vilivyopo kwenye vijiji mbalimbali ili kuwawezesha kunufaika na fursa za kilimo ikiwepo upatikanaji wa mikopo ya kilimo kupitia vyama vya hivyo, huduma za ugani, upatikanaji wa pembejeo, mbolea na mbezu sambamba na uhakika wa soko wakati wa kuuza mazao yao.
Kikao hicho kitafuatiwa na mafunzo kwa maafisa Ugani wa Kata kwa lengo la kuwajengea uwezo Wataalama hao kupata ujuzi wa namna zao hilo linavyiozalishwa kuanzia hatua za awali za maandalizi ya vitalu, uchaguzi wa mbegu, upandaji, jinsi ya kulihudumia shamba, uvunaji na kaushaji kwa kutumia nteknolojia ya kukausha kwa jua
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa