Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Agosti 18.2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Sharifa Yusufu. Nabalang’anya, amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Dakta Samia kwa kutoa ruzuki kwa ajili ya Posho za madaraka za Wakuu wa Divisheni na Vitengo.
Amesema hayo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Waheshimiwa Madiwani cha Taarifa za Robo ya Nne kwa kipindi cha Aprili-Juni 2022/2023 kilichofanyika Agosti 11.2023 kwenye ukumbi Mkubwa wa Mikutano aw Halmashauri.
“Ninamshukuru sana Mhe. Rais Samia, kwa kuamua kubeba jukumu la kulipa posho za Wakuu wa Divisheni na Vitengo moja kwa moja kupitia Ruzuku kutoka Serikali Kuu kila mwezi. Hii inaipunguzia mzigo Halmashauri wa kulipa posho hizo kutoka vyanzo vya ndani vya mapato, hasa kwa Halmashauri yenye mapato kidogo kama Gairo”. Alisema.
Nabalang’anya alisema hapo awali ulipaji wa stahiki hizo za viongozi hao ilikuwa changamoto kutokana na ufinyu wa mapato ya ndani ya Halmashauri hali ambayo ilisababisha kulimbikiza madeni ya tahiki hizo.
Wakuu wa Divisheni wenye sifa wanastahili kulipa posho za madaraka ikiwepo posho ya nyumba, mawasiliano na gharama za bili za maji za umeme.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa