Na. Cosmas Mathiasn Njingo
Morogoro
Septemba 29.2022
Mkuu wa Mkoa wa Morogor Mhe. Fatma Abubakari Mwassa
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Morogoro, wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia kanuni, taratibu na sheria sambamba na kujali mipaka yao ya kiutendaji ili kuepuka kuingilia majukumu ya watumishi wa Umma waliopo chini yao, pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Omari Makame (mwenyemiwani miwani) akifuatilia kongamano la wadau wa kilimo mkoa wa Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa, ametoa rai hiyo wakati akifungua kikao cha Wadau wa Kilimo Mkoa wa Morogoro kilichofanyika Septemba 28.2022 katika ukumbi wa Morena Hotel iliyopo Manispaa ya Morogoro.
“Sasa inawezekana kuna mambo tunaingiliana, hatujui mipaka ya majukumu yetu, hususani Wakuu wa Wilaya wamekuwa wakifanya kazi ambazo siyo zao kwa kuingilia majukumu ya wataalam au watendaji wengine. Hii siyo sawa”. Alisema Mhe. Mwassa.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wadau wa Kilimp Mkoa wa Morogoro
Akitolea mfano kwa Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kuingilia majukumu ya wengine Mhe. Mwassa alisema kumekuwepo na tabia ya baadhi ya Wakuu wa Wilaya kushiriki kuitisha vikao vya Chama cha Mapindizi (CCM) na kusimamia taratibu za chaguzi mbalimbali ndani ya Chama, hali ambayo alisema inaweza kuleta migogoro kati yao na baadhi ya viongozi hususani wagombea wa nafasi hizo.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wadau wa Kilimp Mkoa wa Morogoro
“Kwenye chama sisi ni waalikwa tu, na Mkuu wa Wilaya hana mamlaka ya kuitisha kikao cha chama, isipokuwa kama kuna jambo la kusaidia watakuomba wenyewe, lakini siyo wewe uitishe kikao cha chama eti unapanga uchaguzi”. Aliwambia
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wadau wa Kilimp Mkoa wa Morogoro
Akaongeza kuwa kufuatia hali hiyo, baadhi ya Wahe.Wabunge kwenye maadhi ya Wilaya, wamekuwa wakiwalalamikia Wahe. Wakuu wa Wilaya kuwa wanapanga safu za uongozi ndani ya chama kinyume na taratibu za uchanguzi.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Wadau wa Kilimp Mkoa wa Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa