Na. Cosmas Mathiasn Njingo
Morogoro
Septemba 28.2022
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubar Mwassa, amewataka Viongozi wote ngazi ya Mkoa na Wilaya, pamoja na Wadau wa Kilimo walioshiriki kikao kazi, kuhakikisha wanatekeleza kwa vitendo maazimio ya kongamano la wadau wa Kilimo lengo ikiwa na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakari Mwassa
Ametoa agizo hilo Septemba 28/2022 wakati akifungua kongamano lililo wakutanisha wadau mbalimbali, wakiwepo wa sekta ya kilimo, Mifugo, Uvivu na umwagiliaji, lililolenga kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo na kusababisha uzalishaji wa mazao kupungua.
“Kwa hiyo niwaombe sana, maamuzi tutakayotoka nayo hapa, tukayafanyie kazi, isiwe ni jambo la kuweka kwenye kabrasha, halafu unasahau hapa tulijadiliana nini. Baadae tunarudi kusukumana sukumana katika utekelezaji wa mambo yetu”. Alisisitiza Mhe. Mwassa.
Mkuu huyo wa Mkoa akaongeza kuwa Kikao kazi hicho ni muhimu kwa mustakabali wa kuleta matokeo chanya katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakumba wakulima na wafugaji na kwamba maamuzi yote yatakayo kubaliwa na washiriki wa kondamano hilo ni lazima yafanyiwe kazi bila kuvutana vutana.
Awali, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kufungua kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa, Dakta. Mussa Ali Mussa, aliwaelekeza Watendaji wate wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kuhakiisha wanaandaa mpango mkakati wa kuwaongoza katika kutekeleza maazimio ya yatokanano ya Kikao kazi hicho ili kuwa na muongozo bora wa utekelezaji wa maazimio hayo.
Katibu Tawala Mkoa, Dakta. Mussa Ali Mussa,
“Ninaomba kila mmoja alichukue hili swali, ili tukitoka hapa tuweze kutekeleza yale ambayo tutakuwa tumekubaliana. Swali lenyewe Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ni ‘Nini Kitafuata’ (WHAT NEXT)? Maana yangu nikwamba tunatakiwa kuwa na mpango mkakati wa kuyatekeleza yatokanayo na kongamano hili”. Alifafanua Dakta. Mussa.
Katibu Tawala Mkoa, Dakta. Mussa Ali Mussa,
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa