Na. Cosmas Njingo. GAIRO
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanayosimamiwa na Divisheni za Elimu ya Awali, Msindi na Sekondari yanalenga kuwawezesha walimu kupata mbinu mpya na shirikishi za ufundishaji na ujifunzi ili kuongeza maarifa, umahiri na ujuzi.
Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Mwl. Kulwa Mgallu; amesema matarajio yao mara baada ya mafunzo hayo ni kuongeza kiwango cha ufaulu.
"Baada ya kuhitimu mafunzo haya, Matarajio yetu kama Divisheni ya Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, Walimu wataongeza ujuzi na umahiri kwani wamepata mbinu mpya na shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji". alisema Bi. Mgallu.
Mwl. Mgallu alibainisha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imedhamiria kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinapanda katika ngazi zote kuanzia darasa la Kwanza hadi kidato cha nne.
"Tumekusudia kuhakikisha ufaulu unaongezeka kwa madarasa yote; Mwanafunzi wa darasa la pili afaulu kwenda darasala latatu, walanne afaulu kwenda tano, vivyo hivyo aliyepo kidato cha pili afaulu kwenda kidato cha tatu, hadhalika wa kidato cha Nne afaulu kuingia kidato cha tano.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Gairo,Mwl. Hawa Mponela alisema, matarajio ya walimu hao baada ya kujengewa uwezo ni kuongeza kiwango cha ufaulu kwa asilimia 100.
"Kimsingi Mafunzo haya yamekuja kwa wakati sahihi kabisa, maana tumejifunza mambo mengi hasa mbinu shirikishi ambazo zimetuongezea ujuzi katika ufundishaji na ujifunzaji, na matokeo ya progamu hii ni kuondoa kabisa SIFURI kwa kupandisha ufaulu kwa Asilimia 100" Alisema Mwl. Mponela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa