Na. Cosmas mathias Njingo, GAIRO
Julai 1.2023
Wananchi wa Kijiji cha Leshata,Kata ya Leshata Wilayani Gairo Mkoa wa Morogoro, wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan, kwa kuwaboreshea miundombinu Sekta ya Elimu ya Awali na Msingi baada ya Kijiji hicho kupokea Fedha Kiasi cha Sh.155,800,000 kupitia akaunti ya Shule, za utekelezaji wa Ujenzi wa Nyumba ya Walimu (pacha mbili), Madarasa mawili ya Mfano Elimu Awali na matundu Sita ya Vyoo.
Wametoa shukrani hizo Juni 30 2023 wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Sharifa Nabalang'anya ya kukagua Maendeleo ya utekelezaji wa Ujenzi wa Miradi hiyo kwa Fedha za BOOST.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Ndg. Method Exavery amesema Ujenzi wa miundombinu hiyo utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa Madarasa na madawati uliyodumu kwa miaka mingi hali amabyo ilisababisha kuwepo kwa mazingira magumu ya ufundishaji na kujifunzia.
Naye mmoja wa Wananchi wa Kijiji hicho Bi. Aziza Saidi Kidile, amempongeza Mhe. Rais Samia kwa kutambua changamoto za ukosefu wa nyumba kwa Walimu na kuamua kuwekeza Fedha nyingi za Ujenzi wa Nyumba bora, za kisasa ambazo zitarejesha heshima na hadi ya Walimu kwa kuwa wengi wao wamepanga mitaani kwenye nyumba ambazo hazikidhi hadhi ya Mtumishi wa Umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi. Nabalang'anya amezitaka Kamati za usimamizi wa Ujenzi wa shule zote, Walimu na Mafundi wanaotekeleza Miradi hiyo kuhakikisha majengo yote yanakuwa katika Ubora mashubuti ili thamani ya fedha iendane sanjari na uimara, Ubora na unadhifu wa miundombinu hiyo.
Aidha Mkurugenzi huyo amewaagiza Walimu Wakuu wa Shule ambazo hazina changamoto ya upatikanaji wa maji kuhakikisha wanapanda miti ya kutosha kuzunguka maeneo ya Shule hizo ili kuweka mazingira kwenye hali nadhifu pamoja na kupunguza upepo mkali unaweza kusababisha madhara ikiwepo kung'oa paa za majengo hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa