Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Julai 2023
Wananchi wa Kata ya Chigela wameshiriki zoezi uchimbaji wa misingi ya majengo mbalimbali ya Shule mpya ya Sekondari ya Kata hiyo ikiambatana na uzinduzi wa ujenzi wa miundombinu ya Shule hiyo.
Akiongoza zoezi hilo kuchimba Msingi na uzinduzi wa shughuli za ujenzi wa Shule hiyo Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame kwa niaba ya Wananchi wa Gairo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan kwa kutenga Fedha nyingi zaidi ya Sh. Bilioni Moja kwa ajili ya uboreshaji wa Elimu Awali na Msingi na Elimu Sekondari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Bi. Sharifa Nabalang'anya amewaasa Wananchi hao kuhakikisha wanashiriki katika kusimamia shughuli za ujenzi ili thamani ya Fedha ilingane na ubora wa majengo ya Shule hiyo.
Ujenzi wa Shule Mpya ya Kata ya Chigela utagharimu kiasi cha Sh.528,998,425 Milioni kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa SEQUIP ambapo utahusisha ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa, jengo la utawala, Maabara 3 za Kemia ,Baiolojia na Fizikia pamoja na matundu ya vyoo na uwekaji wa miundombinu ya Maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa