WANAFUNZI 3,907 GAIRO WAFANYA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA
Jumla ya wanafunzi 3,907 wa shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wameanza kufanya Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu Elimu ya Msingi (Darasa la Saba) 2025, sambamba na wenzao nchi nzima.
Mtihani huo umeanza Septemba 10, 2025 na unatarajiwa kuhitimishwa Septemba 11, 2025, ambapo wanafunzi watapimwa katika masomo mbalimbali ili kuhitimisha safari yao ya elimu ya msingi.
Akithibitisha taarifa hizo, Mkuu wa Divisheni ya Elimu Awali na Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mwl. Khadija Mwinuka, amesema kati ya wanafunzi hao, 1,550 ni wavulana huku wasichana wakiwa 2,357.
Mwl. Mwinuka ameongeza kuwa maandalizi ya mtihani huo yamekamilika kwa ushirikiano wa wadau mbalimbali wakiwepo walimu, wazazi pamoja na viongozi wa elimu katika wilaya, ambapo amewahimiza wanafunzi kufanya mtihani kwa kwa umakini na utulivu wa hali ya juu, kuzingatia maelekezo na kujibu maswali yaote ili kufanikisha ndoto zao za kielimu.
Kwa upande Mwingine Afisa Elimu huyo wa Elimu ya Awali na Msingi, amewahimiza wazazi na walezi kuendelea kuwapa watoto wao msaada wa kisaikolojia na mazingira rafiki katika kipindi hiki muhimu cha mitihani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa