Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Septemba 10.2023
Wananchi wa Kata ya Chigela Wilayani Gairo, wamempongeza na kumshukuru Mhe. Dakta Samia Suluhu Hassan, Rais wa awamu ya Sita wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapatia kiasi cha Shilingi 528,945,425.00 (Milioni miatano ishirini na nane, laki tisa arobaini na tano mianne ishirini na tano) za ujenzi wa miundombinu shule mpya ya Sekondari ya Kata hiyo.
Wametoa shukrani zao hivi karibuni waliposhiriki kwenye zoezi la kusafisha eneo na kuchimba Msingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule hiyo ili kuwezesha wataalam kwa Idara ya Miundombinu na Mandeleo vijijini kuweka michoro tayari shughuli za ujenzi kuanza mara moja.
Akimwakilisha Diwani wa Kata ya Chigela ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi, Diwani wa Kata ya Magoweko Mhe. Ibrahim Selubunga Mmbwana alisme, Mhe. Dakta Samia , amefanya jambo kubwa sana la kihistoria kwa Wakazi wa Kata hiyo na kuongeza kuwa; kukamilika kwa ujenzi wa Shule hiyo ya Sekondari ya Kata ni ukombozi kwa wanafunzi wa Vijiji vinavyounda Kata hiyo ya Chigela.
“Kwa niaba ya Diwani wa Kati hii ya Chigela, ambaye ndiye Mwenyekiti wetu wa Halmashaur ya Wilaya ya Gairo, nachua fursa hii kuungana na Wananchi wenzangu kumpongeza na kumshuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuondoa changamoto za Sekta ya Elimu katika Wilaya yetu ya Gairo”. Alisema.
(Jengo la vyumba 3 vya madarasa lililojengwa kwa nguvu za Wananchi)
Akasema “Halmashauri ilipokea jumla ya Shilingi Milioni miatano ishirini na nane ambazo zimeelekezwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Kata ya Chigela, Shule hii itakuwa ya kisasa kabisa kutokana na muonekano wake utakavyokuwa baada ya ujnezi kukamili kwani imebeba miundombinu yote muhimu. Na hii itapunguza adha kwa watoto wetu kutembea umbali mrefu kwenda kata za jirani kupata elimu ya Sekodari”. Alifafanua.
(Jengo la vyumba 3 vya madarasa lililojengwa kwa nguvu za Wananchi)
Naye mwenyekiti wa CCM kata ya Chigela Ndg. Ibrahimu Munga alisema Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inatambua adha mbalimbali zinazowapata Wananchi wa Kata hiyo; hivyo juhudi zinafanyika kuhakikisha Wananchi wanaondokana na kero zinazokuwa kikwazo katika kuleta maendeleo hususani Sekta ya Elimu Awali, Msingi na Sekondari.
Kwa upande wake Mweyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ngiloli Ndg.Dani Samsoni; alisema kuwa Wananchi wa Kata hiyo walipokea kwa heshima kubwa taarifa za mgawo huo wa fedha na kwamba wameamua kujitokeza kujitolea kufanya kazi mbalimbali za awali za kuandaa eneo na kuchimba msingi ili kazi za ujenzi zianze haraka.
“Ninamshukuru sana Mhe Rais kwa kutuona na kusikia kilio chetu Wananchi wa Chigela, hatimaye ametuletea fedhza kiasi cha Sh. milioni 528.945, za ujenzi wa Sekondari Mpya ya Kata. Nasisi tumeamua kutoa shukrani zetu kwa vitendo kuja kujitolea nguvu kazi, ya kusafisha eneo na kuchimba msingi kwa ajili ya shughuli za ujenzi kuanza mara moja”. Alifafanua Ndg. Mwenyekiti huyo wa Serikali ya Kijiji cha Ngiloli.
Kwa kipindi kirefu Kata hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Diwani Nyangasi imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa Shule ya sekondari hali ambayo iliwalazimu Wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule katika kata ya Kibedya na Magoweko.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Divisheni ya Elimu Sekondari Wilaya ya Gairo Bi. Petronila Wakurila, fedha hizo zitatekeleza ujenzi wa Vyumba 8 vya Madarasa, Jengo la Utawala, Maabara 3 za Kemia, Fizikia na Baiyolojia, Maktaba, Jeno la Tehama, Matundu 8 ya vyoo, kuweka mfumo wa maji na kichomea taka.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa