Cosmas Mathias Njingo;
Gairo, MOROGORO.
Disemba 5.2022.
Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa halmashaauri ya Wilaya ya Gairo, limepitisha sharia ndogo ya Halmashauri ya kusimamia udhibiti wa `kwenye mazao ya mimea na Mifugo.
Kikao hicho cha Baraza maalum la Wahe. Madiwani cha kujadili na kupitisha sheria ndogo ya kudhibiti SUMUKUVU kilifakilifanyika Disemba 5. 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuhuddhiriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bw. Dastan Mwendi, wajumbe wa KUU wilaya, Wakuu wa Taasisi za Umma; na Wakuu wa Divisheni mbalimbali wa Divisheni na Vitengo vya Halmashauri.
Mhe. Rahel Nyangasi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo
Akitoa maamuzi hayo Mhe. Nyangasi alisema niwakati muafaka kwa Halmashauri kuharakisha mchakato wa kuandaa rasimu ya Sheria ndogo nyingine za Halmashauri ili zipitishwe kwenye vikao vya kisheria ikiwepo Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango na baaday kuwasilishwa kwenye Kikao cha Baraza la Wahe. Madiwani kwa ajili ya kupitishwa.
“Sheria hii ya kudhibiti SUMUKUVU ipite na iende haraka kwa Waziri mwenya Dhamani, lakini ninakukuagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kupitia Timu yako ya Wataalam na Mwanasheria wa Halmashauri, kwa pamoja mharakishe mchakato wa kuunda rasimu za sheria ndogo ndogo za Halmashauri ili Wahe. Madiwani wazipitishe kupitia Mabaraza yao. Hii itasaidia kusimamia utekelezaji wa Sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa.
Bw. Christopher Mussa Waless, Mratibu wa Kuzuia SUMUKUVU Wilaya ya Gairo akitoa maelezo kuhusu rasimu mpya ya Sheria ndozo za Halmashauri za Kudhibiti SUMUKUVU katika Kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi Disemba 5.2022
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Adv. Waryoba Mussa
Akitoa maoni yake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Omari Makame alisema; kutumika kwa sharia hiyo kutaleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Kilimo na kwamba wajibu wa Wahe. Madiwani hao ni kuhakikisha inatekelezwa katika maeneo yao ili kuongeza tija katika uzalishaji sambamba na kuondoa madhara yatokanayo na SUMUKUVU kwa Binadamu na Mifugo.
Mhe. Jabiri Omari Makame, Mkuu wa Wilaya ya Gairo“Sheria hii ni muhimu sana katika kuleta mageuzi kwenye sekta ya kilimo, niwaombe Waheshimiwa Madiwani kwenda kuisimamia na kuitekeleza kwa vitendo ili kila mdau anayetajwa katika sheria hii awe ni chanzo cha mabadiliko ili tuondokane na madhara yatokanayo na SUMUKUVU”. Alisema Mhe. Makame
Mhe. Makame akalitaka baraza hilo pamoja na Wataalam wa Halmashauri kuharakisha mchakato wa uundaji wa sheria nyingine ndogo ndogo zikiwepo sheria ndogo ya Mfuko wa Elimu na Sheria ndogo ya Utoaji wa Chakula shuleni ili ziweze kutumika katika kuboresha Sekta ya Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa