Na. Cosmas M. Njingo (AFISA MAWASILIANO GAIRO DC)
Vijana Wilayani Gairo wameshauriwa kuwa wabunifu katika kuibua miradi mbalimbali ya kiuchumi waweze kuzalisha mali sambamba na kutumia fursa za mikopo kwa vijana zinazotolewa na Halmashauri badala ya kukaa vijiweni kucheza bao, kunywa pombe na kujiingiza katika vitendo vya kihalifu ambavyo vinaweza kuathiri afya zao.
Ametoa rai hiyo Mkuu wa Wiaya ya Gairo Mhe. Jabir Omary Makame hivi karibuni alipokutana na kikundi cha Rubeho Transporters cha Vijana waendesha boda boda waliopewa mkopo wa pikipiki 10 na Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ili waweze kujiongezea kipato kwa kujiajiri.
“Ushauri wangu kwa vijana wote ni kwamba muache kukaa vijiweni na kupoteza muda pasipo kufanya shughuli za uzalishaji mali, tumieni fursa zilizopo ili mjikwamue kiuchumi kwa kujiunga katika vikundi na kubuni shughuli za kiuchumi ili muweze kuendesha masiha yenu”. Alisema Mhe. JOM.
DC. JOM alisema kuwa Serikali kupitia Halmashauri imekuwa ikitoa fursa za mikopo kwa vikundi mbalimbali vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ambapo alifafanua kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutenga asilimia kumi (10) ya mapato yanayo kusanywa kutoka kwenye vyanzo vya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vilivyo sajiliwa.
“Vijana wenzenu wa Rubeho Transporter waliamua kujiunga katika kikundi wakaomba mkopo Halmashauri kwa kufuata taratibu zote, na baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa kikundi kimesjiliwa na kinakopesheka wakapata asilimia nne (4%) za mapato ya ndani na leo hii wamejikwamuwa”, alibainisha
Rubeho Transporters ni kikundi cha vijana kumi walio ungana kwa pamoja na kupewa mkopo wa Shilingi milioni ishirini na tatu na laki tano (23,500,000) ikiwa ni sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwezesha kikundi hicho kununua pikipiki kumi ambazo zinatumika kibiashara.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Bwana Isaya Mihinzo alisema mkopo huo hauna riba na kwamba marejesho yake yatafanyika katika kipindi cha mwaka mmoja hadi kufikia 2022 ili kutoa fursa kwa vijana wengine ambao wanatamani kutumia fursa hiyo kwa ajili ya kujiari na kupata kipato.
“Katika mwaka wa fedha 2020/2021 moja ya vikundi vilivyonufaika na sharia na kanuni hizi ni kikundi cha Vijana cha Rubeho Transporters kilichopo kata ya Rubeho chenye wanachama kumi, kikundi hiki kilianzishwa mwaka 2020, hivyo Halmashauri ilitoa mkopo wa shilingi milioni ishirini na tatu na laki tano kwa mashariti ya kulipa mkopo huo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja bila riba yoyote”, alifafanua Bwana Mihinzo.
Ilielezwa kuwa hadi sasa kikundi hicho tayari kimesha rejesha kiasi cha Shilingi milioni sita laki tano na ishirini elfu, sawa na shilingi milioni moja, laki tisa na hamsini na nane elfu mia tatu thelathini na tatu na senti thelathini na tatu kwa mwezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa