Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO
Aprili 21. 2025 Wataalam wa Afya na Lishe Wilayani Gairo, wametakiwa kuongeza juhudi za utoaji wa Elimu kwa Umma kuhusu maswala ya Lishe, matumizi sahihi ya vyandarua ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Malaria, pamoja na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kuchangia Damu kwa ajili ya kusaidia wenye uhitaji na upimaji wa Virusi vya UKIMWI ka hiari.
Rai hiyo imetolewa na Ndg. Godfrey Mnzava, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa alipokuwa akitembelea mabanda ya shunguli za Lishe, Malaria, UKIMWI na damu salama wakati wa kukagua na kuweka jiwe la msingi kwenye Zahanati ya Kijiji cha Ng’holonngo Kata yas Madege Tarafa ya Gairo, Aprili 21.2024.
“Hiongereni kwa kazi nzuri mnayoifanya, lakini niwaombe msikae ofisini, tokeni mwende kwa Wananchi mkatoe elimu juu ya umuhimu wa Lishe Bora kwani Mhe. Rais Samia amewekeza Ferdha nyingi katika kuhakikisha afua za lishe zinatekelezwa kikamilifu, hivyo ni bora kuhakikisha mnawafikia Wananchi na kuwapa elimu hiyo”. Alisema Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Akiwa katika banda la kuzuia maambukizi ya Malaria kiongozi huyo alisema Wananchi wanapaswa kufahamu matumizi sahihi ya vyandarua ambavyo vinatolewa na Serikali kwa lengo la kuzuia kuenea kwa ungonjwa huo kwani wapo baadhi ya Wananchi wamekuwa wakitumia vyandarua kwa shughuli tofauti na ilivyokusudiwa huku akitaja matumizi hayo kuwa ni ufugaji wa kuku, uvuvi na wengine kutumia vyandarua kuzuia kuku kuharibu bustani za mboga mboga.
Kuhusu damu salama Kiongozi huyo amewataka Wataalam hao kuweka mikakati na kuongeza juhudi za kuwafikia Wananchi wengi zaidi na kuwapa hamasa ili watambue umuhimu wa kuchangia damu kwa lengo la kupunguza vifo na kuokoa maisha ya Watoto na Wanawake Wajawazito wakati wa kujifungua..
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Gairo Aprili 21.2024 ukitokea mkoani Tanga, ambapo utakimbizwa, kuona, kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kufungua jumla ya miradi 9 yenye thamani ya shilingi 1,594,217,370.12, huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiweka msisitizo katika shughuli za utunzaji wa mazingira na uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kuanzia mwezi Oktoba hadi Novemba 2024.
“Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa