Na. Cosmas Mathias Nningo;GAIRO
Juni 2.2023
Mkurungenzi wa Mipango, Sera na Uratibu (DPP) ofisi ya Rais TAMISEMI Ndg. John Cheyo amewataka Wachumi, Wahandisi Ujenzi na Maagisa Mipango Mkoani, Morogoro kujenga utaratibu wa kuratibu, kufuatilia na kutathimini miradi ya maendeleo kuanzia hatua za awali, wakati wa utekelezaji na baada ili kuongeza ufanisi.
Ameyasema hayo Mei. 31.2033 Wilayani Gairo wakati akifunga Mafunzo ya Siku 3 ya kuwajengea uwezo Maasfa hao kuhusu uandishi wa maandiko ya Miradi ya Maendeleo ya Kimkakati ambayo hutekelezwa nje ya mpango wa bajeti katikawaka husika.
"Nendeni mkaongeze nguvu katika ufuatiliaji na kutathimini utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye maeneo mnayotoka". Alisema Mkurugenzi huyo
Aidha amewataka Wataalam haowa Uchumi, Maafisa Mipango, Wahandisi Ujenzi na Wakuu wa Divisheni ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji kuimarisha ufuatiliaji na tathimini kabla, wakati na baada ya kutekeleza miradi ya Maendeleo ili iendane na thamani ya Fedha inayotolewa na Serikali sambamba na kuleta tija kwa jamii
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa