Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela amewataka Mkuu wa Wilaya, Waheshimiwa Madiwani na watendaji wa Halmashauri kufanya ziara kwenye vijiji na kata ili kutatua kero za Wananchi badala ya kusubiri kufuatwa maofisi.
Ametoa wito huo Juni 14,2021 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
“Mimi nimekuja huku kujitambulisha, lakini nitapanga ziara kutembealea kata zote za Wilaya ya Gairo, na ninyi ni lazima mkhakikishe mnatembea kwenye vijiji na kata mkakutane na Wanachi kwa ajili ya kutatua kero zao huko huko na siyo kusubiri Wananchi wawafuate ofisini”, alisisitiza Mhe. Shigela.
Amesema wananchi wanakabiliwa na kero nyingi lakini wanakosa pakuzifikisha kwa kuwa viongozi wao ngazi ya kata na Watendaji wakuu wa Halmashauri wapo ofisini, na kuongeza kuwa ziara za viongozi hao zitasaidia kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Aliwaonya Watendaji wa Halmashauri hususani wakuu wa idara kuacha mara moja kasumba ya kutokwenda kwenye vijiji na kata kutatua kero za Wazanchi pindi wanapoitwa na Wenyeviti wa Vijiji au Waheshimiwa madiwani ili kutoa ushauri wa kitaalamu na kutatua changamoto zao kwa kisingizo kwamba hawawezi kwenda huko hadi wapate kibali cha Mkurugenzi.
“Sitaki kusikia tena hii kasumba inajitiokeza kwa Mkuu wa idara yoyote, ukipigiwa simu na Mheshimiwa Diwana jadili naye na upange ratiba mara moja ya kwenda kusikiliza na kutoa ushauri wa kitaalamu kisha omba ruhusa kwa Mkurugenzi badala ya kusubiri taarifa ipitie kwa Mkurugenzi ili yeye akupe kibali, kwa kufanya hivyo ni kuchelewesha maendeleo kwa Wananchi” alionya.
Sambamba na kikao hicho cha Baraza la Madiwani Mhe. Shigela alikutana na Wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya soko la ndizi kata ya Magoweko ambapo aliwambia Wanachi Wilayani Gairo kuwa Serikali imajipanga vizuri katikakuhakikisha inashughulikia kikamilifu kutatua kero za Wanachi.
“Nataka kuwa hakikishia kuwa Serikali Mkoani Morogoro imajipanga kikamilifu katika kuhakikisha inawahudumia vizuri Wananchi wa Gairo na kuweka miundombinu imara ya upatikanaji wa huduma bora za kijamii”, Mhe. Mkuu wa Mkoa alifafanua.
Alibainisha kuwa Serikali imetoa fedha za kutosha ili kuwekeza katika sekta ya elimu kwa ajili ya kusaidia elimu bila malipo kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari lengo ikiwa ni kuhakikisha watoto wote wenye sifa za kwenda shule wanapata nafasi bila kikwazo cha kudaiwa ada.
Katika mkutano huo wa hadhara Mheshimiwa Shigela alipiga maruku Wazazi na Walezi kuacha mara mjra tabia ya kuwaachisha masomo watoto wao kwa kisingizio cha michango inayochangishwa mashuleni na kuongeza kuwa michango siyo sehemu ya ada hivyo kushindwa kuchangia siyo isiwe sababu ya kuwaachisha watoto masomo.
“Michango ni makubaliano mnayofanya kwenye vikao vyenu vya maendeleo ya shule, nina agiza kuanzia sasa sitaki kusikia Mwanafunzi yoyote kaacha masomo kwa sababu tu ya michango mliyojiwekea wenyewe, michango yote ipitishwe na Mkurugenzi wa Halmashauri na kisha Mkuu wa Wilaya atoe kibali”. Alisema.
Wilayani ya Gairo imepata bahati ya kuwa wilaya ya kwanza kwa mkoa wa Morogoro kutembelewa kwa mara ya kwanza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro siku chache baada ya kuteuliwa na kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasani na baadaye kukabishiwa ofisi na alieyekuwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Laota Olesare.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa