Na. Cosmas M. Njingo. Gairo Morogoro
Sept.3.2022
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo Mhe. Andrea Sendeha amemwagiza Afisa mifugo wa Mamlaka ya Mji huo kuhakikisha anasimamia swala la ukusanyaji wa mapato kupitia ushuru wa mifugo na ukaguzi wa nyama katika kata ya Mkalama.
Sendeha ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Mamlaka ya Mji Mdogo cha kujadili taarifa za mwezi Julai 2022, kilichofanyika katika Ukumbi Mdogo wa Mikutano wa Halmashauri Septemba 2.2022.
“Ukipita huko mitaani kwenye Kata ya Mkalama mifugo ipo mingi, nyama zipo za kutosha kila mahali, lakini taarifa ya mapato inayotolewa kwenye vikao vyetu haikisi ukweli uliopo kwenye Kata ya Mkalama.” Alisema Mhe. Sendeha.
Katika kipindi cha mwaka wa Fedha unaoanzia Julai Mosi 2022 hadi Juni 30. 2023 Mamlaka ya Mji Mdogo imekisia kukusanya kiasi cha Shilingi 119,000,000 (Milioni mia moja kumi na Tisa) kutoka kwenye vyanzo mbalimbali katika Kata tano (05) za Mamlaka ya Mji, ambapo hadi kufikia mwezi Julai 30 2022 imekusanya kiasi cha Shilingi Milioni Saba, miatisa na thelathini elfu mia Saba (7,930,700) sawa na asilimia 6.66.
Mchanganuo wa Makisio ya makusanyo hayo kwa kila kata umezingatia upatikanaji wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali ambapo kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 Kata ya Magoweko inakisia kukusanya jumla ya Sh.40, 000,000 ambapo hadi kufikia Julai 30 2022 kiasi cha Sh.3, 215, 300 kimekusanywa (8.04%).
Kata ya Gairo ilikisiwa kukusanya kiasi cha Shilingi 30,000,000 ambapo kwa mwezi Julai 2022 imakusanya jumla ya Shilingi 3, 239, 400 sawa na asailimia 10.8. Wakati Kata ya Ukwamani ilipanga kukusanya Shilingi 30, 000,000 anbapo imekusanya shilingi 930,000 kwa mwezi Julai 2022 (3.10%)
Aidha Kata ya Mkalama iliweka makisio ya kukusanyo kiasi cha Shilingi 7,000,000 kufikia June 2023 na kwamba katika kipindi cha mwezi Julai 2022 Kata hiyo imefikia asilimia 4.66 ya makusanyo hayo kwa kukusanya jumla ya shilingi 220, 000.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa