Na. Cosmas Njingo,GAIRO,
JANUARI 27.2023
Watoa huduma ndogo za fedha Wilayani Gairo, wametakiwa kurejesha mara moja fedha za marejesho ya mikopo ya wateja wao, walizoendelea kuwakata kwa makusudi hata baada ya wateja hao kumaliza kulipa deni la mikopo yao.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilayaya Gairo #jabirimakame wakati akifunga mkutano wa Wadau wa Huduma Ndogo za Fedha uliofanyika Januari 24.2023 katika ukumbi mdogo wa Mikutano wa Halmashauri.
"Fedha zote za marejesho ambazo mliendelea kuwakata wateja wenu ingawa tayari walisha maliza kulipa madeni yao, muwarejeshee mara mmoja, hii haikubaliki kwani nikinyume cha taratibu na sheria za huduma ndogo za fedha". Aliagiza
Mhe. Makame akaongeza kuwa kupitia ukaguzi uliofanywa na kamati ndogo aliyoiunda ikijumuisha maafisa kutoka vyombo vya usalama Wilayani humo, kwenye taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha na kubaini mapungufu mengi ikiwepo ukiukwaji mkubwa wa masharti yaliyowekwa katika sheria ya huduma ndogo za kifedha chini ya Benki Kuu ya Tanzania.
Mapungufu mengine yaliyobainika wakati wa ukaguzi huo ni pamoja na kutokuwepo kwa mikataba ya kueleweka baina ya watoa huduma hao na wateja wao, usiri wa mikataba ya ukopeshaji wa fedha, kiwango kikubwa cha makato ya riba na kuzuia Kadi za Benki za Wateja wao kinyume na utaratibu
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Huduma Ndogo za Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BOT), aliwambia wadau hao kuwa sheria ya Huduma Ndogo za Fedha inazitaka Taasisi zinazotoa huduma hizo kutoza riba isiyozidi asilimia 3.5 (3.5%) kwa m,wezi ya kiasi cha Mkopo anachokopa Mteja, lakini sheria hiyo inaikukwa kwa baadhi ya Taasisi kutoza kati ya asilimia 20 hadi 50 kwa mwezi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa