Na Cosmas M. Njingo
Aprili 20
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo imepokea jumla ya pikipiki 24 za Maafisa Kilimo 8 wa vijiji na Kata 15 na 3 za Maafisa ngazi ya halmashauri.
Akikabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame, amewaagiza wataalam hao kuhakikisha wanazitunza pikipiki hizo ili ziweze kuleta matokeo chanya kwa wakulima watakao wafikia na kuwapa huduma mbalimbali za ugani.
"Tunaipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya mama yetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji. Pikipiki hizi zikatumike kwa ajili ya shughuli za ugani ili lengo la Serikali la kuwafikia wakulima na kuwapa huduma za ugani litimie kuleta tija kwa Wakulima". Akisema Mhe. Makame.
Jumla ya Maafisa Ugani 8 ngazi ya vijiji wamepewa pikipiki hizo kati ya 26,ambapo vijiji vilivyo nufaika na mgawo huo ni pamoja na Kisitwi, Kwipipa, Tabu Hotel, Ihenje, Ngogomi, Masenge, Letugu ya na Kitaita.
Aidha kata zilizopata pikipiki hizo ni Gairo, Chigela, Magoweko, Iyogwe, Nongwe, Idibo na Chanjale.
Kata nyingine ni Mandege, Chagongwe, Italagwe, Madege, Mkalama na Leshata
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa