Na. Cosmas Mathias Njingo; GAIRO
Mei 24.2023
(Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima, akisaini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo)
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima, amewataka watendaji wa Taasisi mbalimbali za Umma Wilayani Gairo, kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa uadilifu na weledi, ili ilete tija kwa Wananchi.
Ametoa agizo hilo Mei 24.2023, wakati wa ziara yake ya siku moja ya kujitambulisha kwa Viongozi Waandamizi wa Serikali na Wakuu wa Taasisi za Umma Wilayani Gairo, katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
(Mhe. Kighoma Malima, akipokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo wakati wa ziara yake ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo)
"Utekelezaji na Usimamizi wa miradi lazima uwe katika uadilisfu wa hali ya juu ili matarajio ya Mhe. Rais Samia kwa Wananchi wake yatimie na miradi ilete na tija". Alisisitiza Mhe. Malima.
Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa huyo alikutana na MWenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabiri Makame, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Danistani Mwendi, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Rahel Nyangasi na Wajumbe wa KUU Wilaya.
(Meneje wa Tanesco Wilaya ya Gairo akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya REA na Umeme wa shirika hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima)
Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Dkt. Godbless Luhunga, Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma pamoja na Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo Mhe. Andrea Sendeha.
(Meneje wa Wakala ya Barabara Mijini na Vijijini Ndg. Massala akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa