Na. Cosmas Njingo
GAIRO
JANUARI 13.2023
Wadau wa huduma ndogo za Fedha Wilayani Gairo wametakiwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa Wateja wao kwa kuzingatia Sheria, taratibu, Miongozo na Kanuni za huduma ndogo za Fedha wasiopokea Amana pamoja na kuepuka ukwepaji wa kulipa Kodi za Serikali.
Wito huo Umetolewa na Mkuu wa WIlaya ya Gaior Mhe. Jabiri Omari Makame wakati akifunga Mkutano wa Wadau wa Huduma Ndogo za Fedha uliofanyika Januari 26.2023 katika ukumbi mdogo wa Hamlashauri.
"Tunataka taasisi zote ndani ya Wilaya yetu ya Gairo ziwe zimesajiliwa kwa mujibu wa Sheria na Taratibu zinazoelekezwa na Benki Kuu ya Tanzania, Msajili wa Makampuni Brela pamoja na Tume ya Ushindani (FCC)". Alielekeza Mhe. Makame.
Naye Afisa Mkuu Mwandamizi, Idara ya Usimamizi wa Huduma ndogo za Fedha Benki Kuu ya Tanzania aliwambia Wadau hao kutokujiingiza katika vitendo vya ukiukwaji wa Kanuni za Huduma ndogo za fedha kuepuka adhabu ya faini isiyopungua kiasi cha Shilingi Milioni ishirini na isiyozidi Milioni Miamoja, au Kifungo jela ama adhabu zote mbili kwa wakati mmoja.
Kwa Upande wake Afisa Mlinda Mlaji, Idara ya Kulinda Mlaji Tume ya Ushindani Bw. Emmanuel Nyanza amewataka Viongozi wa Taasisi hizo kuzingatia kanuni zote za utoaji wa huduma kwa kuweka bayana Mikataba baina yao na walaji ambao ni wateja wao lengo ikiwa ni kudhibiti malalamiko yatokanayo na kutokuwepo na mikataba inayoeleweka vizuri kwa walaji.
"Nimuhimu sana kuhakikisha Mikataba baina yenu watoa huduma na wateja ipo wazi na inaeleweka, lakini ni vyema Mteja apewe nakala ya Mkataba badala ya kuificha au kubaki nayo". Alisisitiza Afisa huyo kutoka Idara ya Kumlinda Mlaji kutoka Tume ya Ushindani
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa