Na. Cosmas Mathias Njingo. GAIRO DC
Baraza la Washeshimiwa Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Mkoani Morogoro, limewarejesha kazini watumishi 3 waliokuwa mawesemamishwa kazi kwa tuhuma mbbalimbali za kiutumishi ikiwepo kushindwa kutekeleza majukumu yao kimalifi huku likimsimamiha kazi Mkuu wa Idara ya Afya kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaka na manunuzi ya vifaa vya ofisi vilivyo chini ya viwango.
Hayo yalisemwa na Mhe. Rachel Nyangasi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, wakati akisoma maamuzi ya Waheshimiwa Madiwani baada ya kujigeuza Kamati kujadili maswala mbalimbali ya kiutumishi Mei 20.2022 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri, katika Mkutano wa Kawaida wa Waheshimiwa Madiwani kujadili taarifa za utekelezaji kwa kipindi cha Robo ya Tatu kwa mwaka wa Fedha 2021/2022
"Kwa mamlaka niliyopewa leo tarehe 20/5/2022, ninatangaza kwamba Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, linawarejesha kazini watumishi 3 waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kiutumishi ikiwepo kushindwa kutekeleza wajibu wao kwa wananchi, utoro kwenye vituo vyao kazi pamoja uzembe kazini. Aidha kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani hili leo ninatangaza Rasmi Kumsimamisha kazi Mkuu wa Idara ya Afya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazo mkabili". Alisema Mhe. Nyangasi.
Watumishi hao 3 walio samehewa na kurejeshwa kazini ni pamoja na Ndugu Francis Mbonde Afisa Muuguzi Msaidizi (Afya) aliyepangiwa kiuto cha katika Kazi kata ya Nongwe baada ya kupewa uhamisho kutoka kata ya Mandege, ambapo alitakiwa kuripoti kituo kipya cha kazi lakini hata hivyo hakutekeleza uhamisho huo wa kuripoti kituoni kwake kwa madai kwamba hakuwa amelipwa fedha zake za uhamisho.
Wengine ni Ndugu Godfrey Chigolo (Afisa Mtendaji wa kijiji cha chagogwe) na Ndugu Barnabasi Mkongo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mandege ambao wote kwa pamaoja walikabiliwa na tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi, utoro , uzembe na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kikamilifu. alikuwa akikabiliwa na kosa la kushindwa kusimamia majukumu yake, utoro kazini na kushindwa kusimamia kikamilifu ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika vijiji vya kata yake.
"Baraza limewasamehe na kuwarejesha kazini, na nina muagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kuwaandikia barua ya onyo kali watumishi hao ili iwe fundisho kwa wengine" Alisisitiza Mhe. Mwenyekiti Nyangasi.
Kuhusu kumsimamishwa kazi Mkuu wa Idara ya Afya wa Halmashauri hiyo, Mhe. Nyangasi aliwaambia wajumbe wa Mkutano huo kuwa Baraza limefikia maamuzi hayo baada ya kubaini kuwepo na mapungufu mbalimbali katika mchakato wa manunuzio ya Kompyuta za Mezani na Mpakato 19 kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma ya Afya, ambapo alisema Mkaguzi wa Ndani amebainisha kompyuta hizo hazikidhi sifa na viwango vilivyowekwa na Serikali kwa.
"Baraza hili la Waheshimiwa Madiwani, pia leo tarehe 20/5/2022 linamsimamisha rasmi kazi Mkuu wa Idara ya Afya kwa kosa la kupitisha malipo ya manunuzi ya Komputa 19 za vituo vya kutolea huduma za afya. Kwa mujibu wa Taarifa ya Mkaguzi wa Ndani kati ya kompyuta hizo ni 3 tu mpya ndio zinasifa zinazo takiwa kwa matumizi ya Serikali lakini zilizo salia 16 zote zilishatumika (used), lakini pia kama haitoshi kumekuwepo na malalamiko ya kutumia vibaya madaraka yake ya ukuu wa idara". Alibainisha Mhe. Nyangasi.
Mkutano huo wa Baraza la Waheshimiwa Madiwani wa kujadili Taarifa za Utekelezaji wa Kipindi cha Robo ya Tatu 2021/2022, ulihudhuriwa pia na Mhe. Jabiri Omari Makame Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Ndugu Shabani Sajilo Mwneyekiti wa CCM Wilaya, Highness Munisi, Katibu wa CCM Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa