Na. Cosmas M. Njingio, GAIRO- Morogoro, Nov 3.2021
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro, limewafukuza kazi jumla wa Watumishi 33 kwa tuhuma mbalimbali ikiwepo utoro kazini, kutoa taarifa za uongo ili kujipatia ajira pamoja na kushindwa kuwasilisha vya ufaulu wa kidato cha nne, pamoja na kuwabadilishia muundo watumishi 22 baada ya kujiendeleza.
Tangazo la kuwafukuza kazi watumishi huo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo Mhe. Rachel Nyangasi, wakati wa kikao cha wazi cha Baraza kwa kipindi cha robo ya kwanza ya Julai-Septemba katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022 hilo.
“Leo tarehe 3 mwezi wa 11 mwaka 2021, kwa mamlaka niliyopewa kisheria na Baraza hili, ninatangaza kuwafukuza kazi watumishi 20 kati ya 33 kwa kutoa taarifaza uongo wakati wa ajira zao kwa nyakati tofauti tofauti kupitia vyeti vya kidato cha nne”. Alifafanua Mhe. Nyangasi.
Mwenyekiti Nyangasi alisema uamuzi huo umezingatia hatua zote za kiutumishi katika kuendesha mchakato mzima wa kuwafungulis hati ya mashitaka baada ya kuunda kamati ya uchunguzi ambapo Kamati ilithibitisha shitaka dhidi yao na kuwatia hatiani.
“Naomba ieleweke kwamba tumezingatia taratibu zote kwa mujibu wa kifungu Na.5.11 cha Sheria ya Menejiment ya Ajira katika utumishi wa Umma Toleo la Mwaka 1998, ikiweka sharti la sifa ya kidato cha Nne kama kiwango cha chini cha kuwezesha mtumishi kuwajiriwa katika Utumishi wa Umma”. Mhe. Nyangasi alifafanua.
Watumishi wengine 10 wamejikuta katika sekeseke hilo baada ya kushindwa kuwasilisha vyeti vya ufaulu wa kidato cha Nne ili viweze kuhakikiwa kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali mwaka 2016 ya kufanya uhakiki wa Vyeti vya kufaulu kidato cha Nne, cha Sita na ualimu pamoja na sifa za kimuundo kwa Watumishi wa Umma.
Mhe. Nyangasi alisema “Baraza hili pia limewatia hatiani watumishi 10 kwa kushindwa kuwasilisha vyeti cya kufauli kidato cha nne kinyume na maagizo ya Waraka Na.1 wa mwaka 2004 ili vihakikiwe”.
Kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi (Establishment Circular) Na. 1 wa mwaka 2004, watumishi wa umma wanao ajiriwa na watakao ajiriwa kuanzia tarehe 2 Mei.2004 ni lazima wawe na cheti cha kufaulu mitihani ya elimu ya kidato cha Nne.
Baraza hilo pia lime wafukuza kazi watumishi wengine wawili (2) wa Halmashauri ya Wulaya ya Gairo kutoka idara ya Utawala na Idara ya kilimo waliokuwa wakikabiliwa na shitaka la utoro kazini.
“Kuna watumishi wengine wawili nao Baraza hili limeamua kuwafukuza kazi kwa shitaka la utoro kazini, tunajua wapo watumishi wengi wenye tabia ya utoro hawakai kwenye vituo vyao vya kazi, hawa nao tutawafuatilia endapo tutawabaini hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwepo kuwaondao kazini”. Alisisitiza Mwenyekiti huyo.
Aidha pamoja na mambo mengine Baraza hilo limewadilishia muundo jumla ya Watumishi 22 kutoka Idara ya Utawala, Elimu na Afya ambao wamekidhi vigezo pasipo kuathiri bajeti ya mishara baada ya kujiendeleza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Gairo-Mtaa wa Malimbika, Kata ya Gairo.
Sanduku la Posta: 40, GAIRO
Simu ya Mezani: +255 787730665
Simu ya Kiganjani: +255 717222572
Barua pepe: ded@gairodc.go.tz, info@gairodc.go.tz
Hakimiliki©2018 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Haki Zote Zimehifadhiwa